KATIKA kujiongezea vyanzo vya mapato, staa wa filamu
za Kibongo, Wastara Juma ameamua kujizatiti zaidi kwenye biashara
ambapo sasa amefungua sehemu ya kuoshea magari maarufu kama Car Wash
iliyopo Tabata, Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi wa car wash hiyo aliyoipa jina la Mamii
Car Wash, Wastara alisema ameamua kujiimarisha zaidi kibiashara kwa kuwa
soko la filamu kwa sasa lipo chini na lina mikikimikiki mingi.
“Hakuna cha maana ninachopata kwenye filamu zaidi ya umaarufu tu.
Wakati marehemu mume wangu (Sajuki) alipokuwa hai alikuwa anakimbizana
kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini mimi kama mtoto wa kike,
nashindwa kufuatilia vizuri.
“Kwa sasa nimeamua kujikita zaidi kwenye biashara, filamu nitafanya
lakini mara chache. Hapa nasubiri Ramadhani ianze na ipite, natarajia
kufungua na hoteli hapahapa baada ya mfungo,” alisema Wastara.
No comments:
Post a Comment