Awali, timu hiyo ilikuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke Dar jioni baada ya kumaliza mazoezi ya ufukweni Coco, Oysterbay asubuhi.
Kiungo mpya wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.
Mbrazili huyo, kwa mara ya kwanza akifanya mazoezi na timu hiyo,
alichubuka pembeni mwa goti na kusababisha damu imtoke kabla ya kupatiwa
matibabu.Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, kiungo huyo mara kwa mara amesikika akilalamikia uwanja huo ambao hivi karibuni ulimsababishia majeraha hayo.
Chanzo hicho kilisema kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazili, Maximo, ndiye alipendekeza mabadiliko ya uwanja ambao alidai haujakidhi viwango.
“Maximo alipenda tuendelee na mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari, lakini imeshindikana kutokana na Coutinho kulalamikia uwanja huo kuwa ni mbovu,” kilisema chanzo hicho.
Kiungo huyo, hivi karibuni aliwahi kuliambia Gazeti la kuwa, uwanja wanaoutumia hauna ubora na anacheza kwa tahadahari kubwa ya kuhofia kupata majeraha katika sehemu za mwili wake.
No comments:
Post a Comment