EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 25, 2014

Dida afunguka, simu ndio chanzo cha kuachana na Ezden, 'alinichapa mikanda', azungumzia mpango wa ndoa nyingine


Dida Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani amefunguka Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm  inayoongozwa na Fadhili Haule na kueleza chanzo cha ndoa yake  na Ezden ‘The Rocker’ Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.
Dida ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi mkubwa kati yao ni simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka kuitumia kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao.
 “Tatizo kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa lilikuwa ni simu. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa tuko kawaida, unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo mimi nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha kawaida. Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize…nikamuita, tulikuwa tunaitana ‘mshikaji wangu mshikaji wangu’. Kwa hiyo alikuwa yuko bafuni anaoga, kwa sababu nyumba ni self-contained, kwa hiyo nikawa namwambia ‘duh mshikaji wangu mbona umeweka password?’ yaani kama utani tu, akaniamba ‘aah we iache simu yangu’.” Dida ameiambia Sunrise ya Times Fm.

Wanandoa washikaji, Dida na Ezden (December, 2013)
Amesema Ezden alishikilia msimamo wake kutomuonesha password kitu ambacho kilimpa hisia na wasiwasi kuwa huenda jamaa anamsaliti (anamichepuko) ameficha kupitia simu hiyo na kuanza kuongeza nguvu ya kuomba apewe password ili aondoe wasiwawasi wake lakini hakufaulu zoezi hilo.
Ameiambia Sunrise ya 100.5 Times Fm kuwa kitu kilichomfanya afikirie kuwa ameonewa kwa kunyimwa password ni uhuru aliokuwa nao mumewe huyo wa zamani kupitia application za kidijitali.
Amesema Ezden alikuwa na uwezo wa kuona kila kinachofanyika kwenye simu ya Dida hata  kupata jumbe zinazoenda kwenye simu ya Dida kabla mwenyewe hajazipata.

Dida na Ezden wakifunga ndoa July,2013
“Simu yangu anauwezo wa kushika akakaa nayo, simu yangu anaweza kushika akadownload vitu vya kuweza kufatilia Dida anaenda wapi, Dida anafanya nini. Messages zangu za WhatsApp alikuwa anaweza kupata yeye kabla yangu mimi. Na kingine kikubwa ni kwamba alikuwa anaweza kudownload maongezi ambayo naongea na watu. Lakini hajawahi kukuta maongezi mabaya na watu….Nikiwa Kawe simu yake inamuonesha kuwa Dida yuko Kawe.” Ameeleza.
Hata hivyo, ametaja kuwa wasiwasi wa mumewe huyo wa zamani na mabadiliko yake katika matumizi ya simu yalitokana na ujumbe ambao alikuwa ametumiwa na mwanaume ambaye kwake yeye ni mteja.

Lakini ujumbe huo haukueleweka vizuri kwa sababu kuna kitu anadhani kilimiss kwenye ujumbe huo kilichosababisha ieleweke tofauti (Kama mtu anaechepuka nae).
Ameeleza kuwa alipoendelea kuomba zaidi password na hali ya kutoelewana kuongezeka akajikuta akipigwa vibao na hapo mambo yakazidi kuwa mabaya kwenye uhusiano huo.
“Alinipiga kibao, sio kibao tu, Vibao vya uhakika….baada ya kupigwa mimi nilishikwa na hasira kwa sababu alinipiga na baadae akaona kibao hakitoshi. Akachukua mkanda, mkanda huu wenu wa suruali lakini ulikuwa mzito akawa ananichapa nao ‘kwa nini unataka kupishika vitu vyangu’.
Anasema kutokana na kipigo hicho aliumia kichwani na kuelekea hospitali, lakini aliporudi nyumbani alikuta mwenzake ameshachukua vitu vyote alivyokuwa anavimiliki (alivyoenda navyo).
Alipoulizwa nani alimuacha mwenzake:
“Sitaki kusema nani kamuacha mwenzake kwa sababu mimi ndiye niliomba divorce. Katika maisha ya mwanadamu wanasema mwanamke hauwezi kumuacha mwanaume ila mwanaume anaweza kumuacha mwanamke. Lakini mimi nahisi kama tumeachana.”
Katika hatua nyingine, Dida aliulizwa kuhusu mpango wake wa baadae katika uhusiano wake kama ana mpango wa kuolewa tena.  Alisema hana mpango huo kwa sasa.
“Kwa sasa sina mpango wowote wa kuhusiana na suala la ndoa. Yaani sina na sitegemei. Na kama kuna mtu anafikiria kwa sababu napata maombi mengi sana. Washindwe na walegee. Kwamba labda naweza kusema mwenyezi Mungu amenijalia kuwa nabahati hiyo…Sio kupendwa yaani tuseme, unajua binadamu anakupenda mwingine anakujaribu. Sasa hivi watanifuata wanaume wengi sana kila mmoja atakuja kwa sampuli anayoijua yeye. Huyu atajifanya yeye ndiye ana mahaba kuliko Yule. Mwingine anasema ‘atapigaje mwanaume?’ kumbe yeye ndiye mdundindaji kwelikweli kuliko hata yule.
“Sitaki kuja kujutia maisha yangu, sitaki kuja kujutia maamuzi yangu. Huwa nafanya kitu kwa kuangalia mbele zaidi. Mimi nina biashara zangu, nina maisha yangu. Namshukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja. Kwa hiyo nahitaji mtoto wangu awe na maadili fulani hivi ambayo ya kusema kwamba huyu ni mama..nahitaji kumsomesha, nahitaji awe hivi. Lakini sitaki mwanangu asipate matatizo haya ambayo labda mama yake nimepitia. Lakini hii yote nasema ni ujasiri. Nasema Mwenyezi Mungu labda ananionesha njia.” 
CHANZO NI TOVUTI YA TIMES FM

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate