Uongozi wa Yanga umekamilisha kila kitu kuhusiana na nyumba
watakayoishi washambuliaji wake Jaja na Coutinho raia wa Brazil eneo la
Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Jaja na Coutinho waliouomba uongozi wa Yanga waishi Kariakoo karibu
na makao makuu ya klabu yao badala ya kupelekwa kwa ‘wanene’, Masaki au
Oysterbay.
|
JAJA&COUTINHO WAKIWA MAZOEZINI NA KIKOSI CHA YANGA... |
Habari za uhakika zinasema tayari Yanga imelipa nyumba hiyo na
ilikuwa katika hatua za mwisho za ukarabati.
“Kuna mambo kadhaa ya kurekebisha ili wakae katika hali nzuri
kabisa, ila masuala ya kodi yamekamilika,” kilieleza chanzo ambacho kinasimamia
nyumba watakayoishi, kisha kikaendelea:
“Uongozi wa Yanga umekuja kumalizana nasi na sasa ni suala la wao
kuingia tu, ila tuliwaomba kufanya ukarabati.”
Makocha Marcio
Maximo na msaidizi wake, Leonaldo Leiva wao wataishi Masaki katika nyumba
tofauti.
No comments:
Post a Comment