Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI wawili wa Yanga, raia wa Brazil, wameushangaza uongozi wa klabu hiyo baada ya kusema wanataka kuishi eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santana ‘Jaja’,
wameuambia uongozi wa Yanga wasingependa kuishi sehemu ambazo
zinajumuisha matajiri au zinazoonekana za ‘uzunguni’.WACHEZAJI wawili wa Yanga, raia wa Brazil, wameushangaza uongozi wa klabu hiyo baada ya kusema wanataka kuishi eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Makocha wao Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonardo Neiva, wanaishi eneo la Masaki jijini Dar ambalo linajumuisha walionazo.
Jaja na Coutinho wanasema wangependa kuishi karibu na klabuni angalau umbali wa kutembea dakika kadhaa kabla ya kufika.
Makao makuu ya Yanga yapo Kariakoo katika makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam, maana yake Wabrazili hao wamekubali kuishi ‘Uswahilini’ ambako kuna ‘masela’ na watu wengi wa mpira.
Mmoja wa marafiki wa Kocha Maximo, amelieleza Championi Ijumaa kuwa, Jaja na Coutinho wataishi pamoja lakini maeneo ya Kariakoo.
“Kweli, kocha kaniambia wachezaji wake wamezungumza na uongozi wa Yanga kwamba wanataka kuishi karibu na klabu. Awali ilionekana kama Yanga waliingia hofu, lakini wamekubaliana nao.
“Mchakato wa kuwapatia nyumba umeanza na ndani ya siku nne hadi tano watakuwa wamekabidhiwa sehemu wanayotakiwa kuishi,” kilieleza chanzo.
Uongozi wa Yanga umekuwa ukitaka kukamilisha kwanza sehemu ambayo wataishi wachezaji na makocha wake ndiyo inaweza kuzungumzia suala hilo.
Jaja na Coutinho wamekuwa gumzo na watu wengi wamekuwa tayari kuwaona wakicheza ili kupima uwezo wao kama watakuwa msaada Yanga.
Yanga imeajiri Wabrazili wanne kwa wakati mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa ligi huku ikiwa imepania kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment