EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 23, 2014

LULU AMMWAGIA DOLA DK. CHENI


CHANZO GLOBAL PUBLISHERS
MUIGIZAJI mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ juzikati alimsapraizi staa mwenzake wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ pale alipomfuata mbele na kummwagia Dola za Marekani kiasi ambacho hakikujulikana mara moja.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ akimlisha keki Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Lulu alifanya tukio hilo mbele ya watu kibao, katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa (birthday party) ya Dk. Cheni ikiwa ni pongezi zake kwa staa huyo kufikisha miaka kadhaa tangu alipoiona dunia.
Tukio hilo lililomshtusha Dk. Cheni lilitokea Julai 20, 2014 kwenye Ukumbi wa Ngorongoro uliopo ndani ya Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Dk. Cheni aliambatanisha na shughuli ya kuwafuturisha mastaa wenzake na wadau mbalimbali wa sinema Bongo katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Dola alizotunzwa D.k Cheni.
MWANZO WA TUKIO
Ilidaiwa kuwa, Dk. Cheni kwa kuwa aliamua kuitumia nafasi ya kufuturisha siku hiyo na kusherehekea bethidei yake, alijipanga vilivyo kuhakikisha kila mhudhuriaji anafurahia uwepo wake kwenye shughuli hiyo.

Miongoni mwa mastaa waliohudhuria mbali na Lulu ni pamoja na msanii wa nyimbo za kughani mashairi, Mrisho Mpoto, Vincent Kigosi ‘Ray’, Salum Mchoma ‘Chiki’, William Mtitu, Jacob Stephen ‘JB’ na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Wengine ni mkongwe kwenye Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Halima Yahya ‘Davina’, Wastara Juma, komediani Hemedi Maliyaga ‘Mkwere’, Kulwa Kikumba ‘Dude’, mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha (anayelishwa keki) na wengine wengi.
Keki yenye kuonyesha kazi azifanyazo Dk Cheni.
ILIKUWAJE?
Ni baada ya futuru kumalizika ndipo wakati wa shamrashamra za bethidei zilipounga ambapo Chiki aliyebeba jukumu la u-MC aliwatangazia watu kwamba, miaka kadhaa nyuma, tarehe 20, Julai, Dk. Cheni alizaliwa jijini Dar es Salaam.
FURAHA, PONGEZI
Kuanzia hapo, furaha za kumbukumbu hiyo ziliibuka na kwa vile watu walikuwa wameshiba, waliweza kumpa pongezi Dk. Cheni kwa kumfuata mmojammoja alipokuwa amesimama na mke wake, Sabra wakitumia staili mbalimbali kwa kila mmoja alivyotaka lakini bila kuvunja maadili.
Mwanamuziki Prof. Jay akilishwa keki na Dk Cheni kwa niaba ya wasanii wa Hip Hop.
Wengi walimpongeza kwa kumkumbatia au kumpa mkono wa heri ulioambatana na zawadi mbalimbali zikiwemo fedha.
LULU ASIMAMA, AENDA KWA DK. CHENI
Lulu ambaye amezoea kumwita Dk. Cheni baba, naye alisimama na kumfuata ‘mtoto’ Cheni ili kumtunza kwa alichonacho.
Macho ya wengi yalitarajia kumuona Lulu amebeba mzigo wa zawadi lakini walipogundua hana, waliamini angetuza kwa noti za ‘Msimbazi’ ambazo zinatumika Bongo, matokeo yake akaanza kuchomoa dola katika ‘waleti’ yake ya kike na kumtupia.
Dk Cheni akimlisha keki mtoto wake.
MPOTO AJIBU MAPIGO
Kama waliambiana, baada ya Lulu kuonesha jeuri hiyo ya fedha tena zenye hadhi ya kimataifa, Mpoto naye alichomoa waleti yake na kutoa dola kisha akaenda mbele kumpa Dk. Cheni huku watu wakishangilia.
Msanii wa filamu, Lulu,  akichukua chakula.
DK. CHENI ATOA NENO
Baada ya kuona zawadi hiyo, Dk. Cheni ambaye alivaa kanzu yenye  rangi ya maji ya maharage alijikuta akizidiwa na furaha kiasi cha kukaribia kumwaga machozi.
Katika kuonyesha furaha yake, Dk. Cheni alifunguka: “Jamani Lulu utaniua baba yako. Ni mambo gani hayo unanifanyia ya kushtukizana?”
Mwigizaji Vincent Kigosi ‘’Ray’’ akitoa zawadi kwa Dk
LULU ASAKWA NA MAPAPARAZI
Baada ya shughuli hiyo kumalizika, mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko walimfuata Lulu na kumuuliza dola alizompa Dk. Cheni zina thamani ya shilingi ngapi za Kitanzania.
Hata hivyo, nyota huyo alikataa kuweka wazi akisema ni siri ya aliyepewa.
“Hiyo ni siri ya Dk. Cheni mwenyewe, mimi nitasema nini sasa jamani?”
Mapaparazi walimfuata Dk. Cheni na kumuuliza ambapo aliminya idadi kamili ya fedha alizotoa Lulu na Mpoto akisema ni siri yake na mke wake.
Dk Cheni, na ‘crew’ yake, wasanii na waandishi wa habari.
Tunampongeza Dk. Cheni kwa kuadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, tunamtakia kila la kheri katika kazi za mikono yake na familia yake kwa jumla – MHARIRI. Imeandikwa na Musa Mateja, Shakoor Jongo na Shani Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate