JESHI la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam linawashikilia watu
nane na kuwahoji kuhusu tukio la kupatikana kwa viungo vya binadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, Bunju B Julai
21, mwaka huu ambapo mifuko ya plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya
viungo vya binadamu iligundulika.
Polisi walipata taarifa za tuki hilo kutoka kwa wasamaria wema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, polisi walipofika eneo la tukio waligundua mifuko ipatayo 85 yenye viungo vya binadamu vilivyokaushwa na kukakamaa vikiwemo vichwa, miguu, mikono, mioyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu.
Katika eneo hilo, pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.
Baada ya tukio hilo, viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kuwa viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika Maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari IMTU jijini Dar na hivyo polisi wamewakamata na sasa wanaendelea kuwahoji watu nane ambao wanasadikiwa kuhusika na miili hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU.

Waandishi wakifuatilia tamko la Kamishna Kova kuhusiana na tukio la viungo vya watu kukutwa eneo la Bunju.
Jeshi la Polisi limesema litamuhusisha
Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya kukamilika uchunguzi,
jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi ili
sheria ichukue mkondo wake.
Kamanda Kova amewaomba wananchi kuwa watulivu na wasiwe na wasiwasi wakati upelelezi ukiendelea.
(PICHA / HABARI: MAKONGORO OGING', HARUNI SANCHAWA NA GABRIEL NG'OSHA / GPL)
No comments:
Post a Comment