HAPATOSHI!
Mastaa wanaokimbiza katika anga la muziki wa Bongo Fleva, wanatarajia
kuchuana vilivyo kulipamba Tamasha la Usiku wa Matumaini katika Uwanja
wa Taifa, Agosti 8, mwaka huu.
Akizungumza na Risasi Vibes, mratibu wa tamasha hilo ambalo linafanyika kwa awamu tatu mwaka huu, Luqman Maloto aliianika listi ya mastaa hao huku akiahidi kuwa itazidi kuongezeka kadri siku zinavyozidi kusonga.
“Mpaka sasa kila kitu kinakwenda sawa, zimesalia wiki mbili tu na naamini wale mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva watapata kile wanachokihitaji siku hiyo kutokana na mastaa watakaokuwepo kukamua mwanzo mwisho, miongoni mwao ni pamoja na Meninah, R.O.M.A, Shilole, Madee, Juma Nature na kundi zima la TMK wanaume Halisi na wengine kibao ambao listi kamili itaendelea kutoka katika magazeti pendwa.
Akimzungumzia mkali wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘R.O.M.A Mkatoliki’, Maloto alisema kuwa rapa huyo atakuwepo kuwainua mashabiki wote wanaopenda muziki wa Bongo Fleva.
“Ataliamsha jukwaa kwa kupiga nyimbo ambazo kwa namna moja zimetokea kupendwa na mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya kama Mechi za Ugenini, Tanzania, Mechi na hii ya sasa hivi Karibu Kwenye Karamu (K.K.K) na nyingine kibao ambazo zitakuwa kama sapraizi kwa mashabiki.
Maloto aliongeza kuwa Rais wa Manzese Hamad Ally ‘Madee’ atakuwepo kuhakikisha Bongo Fleva inalitawala jukwaa kwa kuwachezesha mashabiki kwa kupiga nyimbo zake zote kali kwa staili tofauti.
“Atawadhihirishia mashabiki kwa nini anaitwa Rais wa Manzese. Mashabiki wategemee kusikia na kucheza siku hiyo nyimbo zote kali kama Pombe yangu, Niskize, Hip Hop Haiuzi, Tema Mate Tuwachape na nyingine kibao ambazo zitaacha gumzo siku hiyo.”
Kuhusu Meninah ambaye amekuwa akifanya maajabu jukwaani katika shoo zote anazopiga kutokana na uwezo wake wa kuimba na kucheza kwa kulitawala jukwaa, Maloto alisema atakamua mbaya.
“Kuonesha kuwa mwaka huu ni wa mabadiliko kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Matumaini mashabiki watamuona Meninah akipafomu nyimbo zake kali kama Shaghala Baghala, Kacopy Kapaste, Dream Tonight na nyingine kibao ambazo zitakonga nyoyo za mashabiki wote watakaofika siku hiyo.”
SHILOLE
Akimzungumzia diva wa muziki wa mduara nchini, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Maloto alisema mashabiki wategemee ushindani mkubwa siku hiyo kwani mwanadada Shilole ataungana na Meninah katika kuhakikisha wanamfunika diva wa muziki kutoka Nigeria ambaye anatamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade.
“Sidhani kama Shilole atakubali kufunikwa kirahisi na Yemi Alade kutoka Nigeria. Atahakikisha mashabiki wake wote anawapa shoo ya kufa mtu kwa kuimba nyimbo zake zote kali zinazotamba kama Chuna Buzi, Paka la Baa, Lawama, pamoja na huu mpya wa Namchukua huku akifanya mikogo ya maana jukwaani.”
Usiku wa Matumaini umedhaminiwa na Vodacom, E.FM, Pepsi, Clouds FM, Azam TV, Times FM pamoja na SYCORP.

No comments:
Post a Comment