EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, July 31, 2014

TAMASHA LA MATUMAINI 2014, MASTAA WAELEZA WATAKAVYOKAMUA TAIFA

Stori: Centre Spread
ITAKUWA balaa! Siku chache kuelekea kwenye Tamasha la Matumaini, Agosti 8, mwaka huu, mastaa kibao watakaolipamba jukwaa litakalofungwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar, wameeleza jinsi gani
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade.
Yemi Alade
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria ambaye huwa habahatishi, amesema: “Nitawapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo zangu zote kali ikiwemo iliyojizolea umaarufu kila kona ya Afrika, Johhny. Mashabiki wategemee kumuona Yemi akimaliza. Kati ya nyimbo ambazo nitazipiga ni Tangerine, Johnny, Bamboo, Birthday, Ghen Ghen Love na nyingine kibao.”
Mzee wa Dushelele, The Single Boy, Ali kiba akipozi.
Ali Kiba
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Mashabiki wengi ‘wamenimiss’, Agosti 8 itakuwa maalum kwa ajili yao. Wategemee ngoma kali kibao kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva niliyerudi kupangusa kiti changu na kukikalia,
“Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni  Mwana na Kimasomaso.”

Malkia wa 'Chuna Buzi', Shilole.
Shilole
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu, hakuna anayebisha kwamba najua kuimba na kukitumia vyema kiuno changu. Nitazipiga Chuna Buzi, Paka la Baa, Nakomaa na Jiji, Lawama na hii mpya ya Namchukuwa.”watakavyolishambulia jukwaa.
Mkali wa Hip Hop Bongo, R.O.M.A mkatoliki ndani ya ofisi za Global.
R.O.M.A
“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao kama Tanzania, Mechi za Ugenini, Pastor, Mr. President pamoja na hii mpya ya Karibu Kwenye Karamu (KKK).
Navy Kenzo.
Navy Kenzo
“Tutawapagawisha mashabiki kwa staili ya Bokodo iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa. Ngoma kama Cheza Kizembe, Usinibwage, Chelewa (Bokodo) na hii mpya ya Aiyola ndizo zitakazosisimua zaidi siku hiyo.”
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Nature akipozi.
Juma Nature
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay Dee, Kama Jana.”
Scorpion Girls, Isabela Mpanda(kushoto) na Jini Kabula wakipozi.
Scorpion Girls
“Sisi huwa hatubahatishi, unapomuona sehemu Isabela na Jini Kabula ujue timu nzima ya Scorpion Girls imetimia. Tutacheza na kuwaimbia nyimbo zetu kama Tanzania, Watuache na  nyingine kibao.”
Mzee wa Tema Mate Tuwachape, Madee ndani ya ofisi za Global.
Madee
“Pale taifa nitakwenda kudhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, noma saaana!”
'La Diva', Meninah zao la Bongo Star Search akipozi.
Meninah
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate