IM looking for my Johnny
Where is my Johnny...
Johnny oooh
Do you know Johnny...question
Kiitikio hicho ndiyo habari ya mjini kwa sasa na good news ni kwamba staa wa wimbo huo, Yemi Alade wa Nigeria anadondoka Bongo kwa mara ya kwanza kuungana na listi ndefu ya wasanii wa nyumbani kulipamba Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8, mwaka huu (Nanenane).
MJUE ZAIDI
Mwanadafada huyu ambaye alizaliwa Machi 13, 1989, anauweza muziki na kuthibitisha hilo alianzia kanisani akiwa mwanakwaya. Kukubalika kwake kulianza mwaka 2009 aliposhinda katika onesho la vipaji lililojulikana kama Peak Talent.
Wimbo wake wa kwanza kuachiwa ulikuwa Fimisile aliomshirikisha eLDee na baada ya kuuachia, alijizolea mashabiki wengi katika kipindi kifupi.
SHOO YA MATUMAINI
Mkali huyo kutoka Jimbo la Abia pande za Nigeria, ameahidi kupiga shoo kali ambayo itafuta historia ya baadhi ya wasanii wa nchini kwao waliowahi kukanyaga ardhi ya Jakaya (Bongo).
Atazipiga ngoma zake kali zikiwemo Tangerine (mpya) na Johhny ambazo zinabamba kutokana na staili yake ya kuimba na kucheza sambamba na mashabiki jukwaani.
MASTAA WA BONGO
Listi ya mastaa kutoka Bongo itaongozwa na Ali Kiba, R.O.M.A, Madee, Juma Nature (na kundi zima la Wanaume Halisi) na wengine kibao ambao watatangazwa hivi karibuni.
TUJIKUMBUSHE MWAKA JANA
Mwaka jana tamasha hilo lilifanyika Julai 7 (Sikukuu ya Sabasaba) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Mwaka huu atakuwa nani? Endelea kufuatilia magazeti Pendwa yatakujuza.
Burudani ya mwaka jana ilikuwa ni asilimia mia kwani mbali na michezo mbalimbali kulipamba tamasha hilo kama mechi wa wabunge wa Simba na Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie, staa kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ alitimba uwanjani na kuchuana vikali na Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusababisha burudani ya kutosha.
MWAKA HUU SASA
Ukiachana na mkali huyo kutoka Nigeria, katika upande wa mpira wa miguu, wabunge wa Simba watakipiga na wenzao wa Yanga bila kusahau mpambano mkali wa ngumi kati ya mabondia wanaotisha kwa sasa, Mada Maugo na Thomas Mashali. Tamasha hili linawajia kwa udhamini wa Vodacom, Pepsi, Azam Tv, E.FM na Times FM.

Julai 2012, Yemi aliachia video ya wimbo mwingine uitwao Ghendhenlove.
Mpaka sasa ameshapiga kolabo na wanamuziki wakubwa wakiwemo Dipp, Ice Prince, eLDee, M.I, Sauce Kid, Shank, Sir Shina Peters, Waje, Wizkid, Yemi Sax na kufanya kazi na maprodyuza wakubwa wakiwemo OJB Jezreel, eLDee, E. Kelly, IBK, Major One, Sizzle Pro, DJ Klem, Bigfoot, Shadybizniz, Dtunes, Garth, na Flip Tyce.

Mwanamuziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki naye atashusha burudani ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
Kama hiyo haitoshi, Yemi ana mkataba na Kampuni ya Effyzzie Music
Group na ndiyo waliomuwezesha kutoa albamu ya Johnny aliyoitengeneza
chini ya Selebobo.SHOO YA MATUMAINI
Mkali huyo kutoka Jimbo la Abia pande za Nigeria, ameahidi kupiga shoo kali ambayo itafuta historia ya baadhi ya wasanii wa nchini kwao waliowahi kukanyaga ardhi ya Jakaya (Bongo).
Atazipiga ngoma zake kali zikiwemo Tangerine (mpya) na Johhny ambazo zinabamba kutokana na staili yake ya kuimba na kucheza sambamba na mashabiki jukwaani.
MASTAA WA BONGO
Listi ya mastaa kutoka Bongo itaongozwa na Ali Kiba, R.O.M.A, Madee, Juma Nature (na kundi zima la Wanaume Halisi) na wengine kibao ambao watatangazwa hivi karibuni.
TUJIKUMBUSHE MWAKA JANA
Mwaka jana tamasha hilo lilifanyika Julai 7 (Sikukuu ya Sabasaba) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Mwaka huu atakuwa nani? Endelea kufuatilia magazeti Pendwa yatakujuza.
Burudani ya mwaka jana ilikuwa ni asilimia mia kwani mbali na michezo mbalimbali kulipamba tamasha hilo kama mechi wa wabunge wa Simba na Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie, staa kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ alitimba uwanjani na kuchuana vikali na Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusababisha burudani ya kutosha.
MWAKA HUU SASA
Ukiachana na mkali huyo kutoka Nigeria, katika upande wa mpira wa miguu, wabunge wa Simba watakipiga na wenzao wa Yanga bila kusahau mpambano mkali wa ngumi kati ya mabondia wanaotisha kwa sasa, Mada Maugo na Thomas Mashali. Tamasha hili linawajia kwa udhamini wa Vodacom, Pepsi, Azam Tv, E.FM na Times FM.
No comments:
Post a Comment