Mkurugenzi
wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati), ambaye kampuni yake
inaandaa tamasha hilo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais
wa Chama cha Ngumi za Kulipwa nchini (T.P.B.O) Yasin Abdallah
(katikati) ambao ndiyo wasimamizi wa pambano la Maugo na Mashali katika
tamasha hilo, akizungumzia pambano hilo.
Meneja
Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) na
Mkurugenzi Chuo cha Uandishi wa Habari, Biashara na Utawala cha Mlimani
kilichopo Mbezi Kwa-Msuguri jijini Dar, Hassan Ngoma (kushoto kwa
Mrisho), wakifuatilia kinachoendelea.
Mwakilishi
na Rais wa Bongo Muvi Unity, Steve ‘Nyerere’, akielezea jinsi
watakavyowagaragaza wasanii wa Bongo Fleva kwenye pambano la soka.
Mwakilishi
wa timu ya Bongo Fleva, Inspector Haruni, akijibu mapigo kwa kueleza
jinsi watakavyowararua Bongo Muvi Unity. Kushoto ni mratibu wa tamasha
hilo, Luqman Maloto, na Eric Shigongo.
Mbunge Hamisi Kigwangala anayeiwakilisha timu ya wabunge wa Simba akieleza jinsi walivyojiandaa kuwaadabisha wabunge wa Yanga.
Msanii
wa filamu, Jacob Steven 'JB', ambaye atachapana na msanii mwenzake,
Issa Mussa 'Clouds 112', akichimba mkwara jinsi atakavyomkalisha msanii
huyo.
Clouds
112 (kushoto) akimchimbia mkwara JB ambaye aliishia kumuangalia
kidharau na kusema anasubiri siku ya Agosti 8 katika Uwanja wa Taifa.
WASHIRIKI wa ‘Tamasha la
Usiku wa Matumaini’ leo wametambiana kwenye mkutano na vyombo vya habari
uliofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza, Afrika-Sana jijini Dar es
Salaam.
Katika mkutano huo wa tamasha hilo la
burudani mabondia, Mada Maugo na Thomas Mashali, kila mmoja amejitapa
kumchakaza mwenzake katika pambano hilo huku Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis
Kigwangala, aliyewawakilisha wabunge wa timu ya Simba alijitapa timu
yake kuwamaliza Yanga.
Msanii wa Filamu za Maigizo, Issa Mussa
'Clouds 112' ambaye katika tamasha hilo atachapana makonde na Jacob
Steven 'JB' katika mchezo wa 'boxing' wote wameahidi kutifuana
'kinomanoma'.
Rais na mwakilishi wa timu ya Bongo Muvi
Unity, Steve Mengere 'Steve Nyerere', alitamba timu yake kuigaragaza
timu ya Bongo Fleva ambapo mwakilishi wake, Haruni Kahena 'Inspector
Haruni', alisema wao ndio watakaoibuka kidedea na kuwapiga Bongo Muvi
Unity kwa mabao 7-1 kama walivyofanywa Wabrazil na Ujerumani wiki
iliyopita kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 8
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo huu
utakuwa ni mwaka wa tatu mfululizo kufanyika likiandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.
(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL. )
No comments:
Post a Comment