YETU macho
katika hili; Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa kiungo
mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, ambaye juzi jioni alijiunga na
Simba kudai kuwa atapambana na Wanajangwani hao kuhakikisha haki yake
inapatikana.
Maneno hayo ya Okwi yamekuja baada ya kudai kuwa Yanga imevunja naye
mkataba kisha kumfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kwa madai ya kushindwa kuzingatia makubaliano yake na klabu hiyo
kwa mujibu wa mkataba wake.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi atahakikisha anapambana Yanga
hadi hatua ya mwisho kuhakikisha anapata haki yake.Alisema klabu yoyote
ile inapoingia mkataba na mchezaji inatakiwa kumlipa fedha zake zote za
usajili kwa mujibu wa makubaliano na siyo kumzungusha na kufanya mambo
yake kama viongozi wake wanavyotaka.
“Sina hofu kabisa juu ya jambo hili, naamini haki itapatikana kwa
sababu hayo ambayo Yanga wananipakazia hayana ukweli wowote na kama kuna
ukweli basi kutakuwa na sababu.
“Hata hivyo kwa sasa haina haja ya kuongea mambo mengi ila jambo la
msingi ambalo ningependa kusema ni kwamba, nipo tayari kusimama sehemu
yoyote ile juu ya jambo hili ili kuhakikisha haki yangu inapatika.
“Hata kama TFF na Fifa watanihitaji leo hii nitasimama mbele yao na
kutoa ushahidi wangu juu ya jambo hili,” alisema Okwi ambaye Yanga
imeachana naye akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile du Sahel ya nchini Tunisia ambayo alikuwa na matatizo nayo.
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile du Sahel ya nchini Tunisia ambayo alikuwa na matatizo nayo.
No comments:
Post a Comment