EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 19, 2014

Jaja amfunika Okwi kwa mshahara


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Geilson Santos ‘Jaja’.
Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Geilson Santos ‘Jaja’, amempiku kwa mara nyingine mshambuliaji mpya wa Simba, Emmanuel Okwi, safari hii ikiwa ni katika mshahara wa mwezi.Siku chache zilizopita, Jaja amekuwa ndiye mchezaji gumzo zaidi hasa baada ya kufunga mabao mawili wakati Yanga ilipoivaa Azam FC na kuitwanga kwa mabao 3-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.

Umaarufu huo wa Jaja ulifanya amfunike Okwi huku mashabiki wa Yanga wakiona wamepata mbadala wa kuwapoza baada ya Okwi kurejea Simba, ghafla.

Kwa mara nyingine, Jaja amezidi kung’ara baada ya mshahara wake anaochota kwa mwezi Yanga kuwa unazidi ule wa Okwi kwa dola 100 (Sh 168,000).
Simba inamlipa Okwi dola 2,500 (Sh milioni 4.2) na imeelezwa inaweza kumuongeza wakati wa kuingia mkataba mpya.Yanga inatoa dola 2,600 (Sh milioni 4.4) kwa Jaja ambaye mshahara wake unaendana na ule wa Andrey Coutinho.
Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ndiye mchezaji anayeongoza kwa mshahara ‘rundo’ kwa wachezaji wote wa Yanga na Simba kwa kuwa kwa mwezi analamba dola 3,000 (Sh milioni 5).
Wageni wengine ni Hamis Kiiza anayechukua dola 2,500, sawa na Mbuyu Twite, mwenye uraia wa Rwanda lakini akiwa na asili ya DR Congo.

Kwa upande wa Simba, Okwi ndiye anaongoza kwa mshahara huo wa dola 2,500 akifuatiwa na nahodha Joseph Owino anayepokea dola 2,000 (Sh milioni 3.4), anafuatiwa na Paul Kiongera (dola 1,500), halafu Amissi Tambwe na Pierre Kwizera wote raia wa Burundi ambao kila mmoja analamba dola 1,000 (Sh milioni 1.7).
Mishahara ya wachezaji wa Yanga imeonekana kuwa juu zaidi kuliko wale wa Simba na inaonekana Simba ambayo imepata uongozi mpya, inaanza kujipanga.
Kabla ya kuingia kwa uongozi mpya, wachezaji wa Simba walikuwa wakipokea mishahara ya chini zaidi lakini tayari wameanza kujitutumua.Yanga walianza kuboresha mishahara ya wachezaji wao mapema na wamekuwa wakisisitiza wataendelea kufanya hivyo.
Timu hizo kongwe mbili na Azam FC ndizo zinaonekana kuwa na mishahara mikubwa kwa wachezaji wake wa kigeni na angalau wale wa nyumbani.
CREDIT: CHAMPIONI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate