EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 19, 2014

LAANA YA KANUMBA YAIMALIZA BONGO MUVI

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
IMEVUJA! Kuvunjika kwa Kundi la Bongo Movie Unity kumedaiwa kuwa ni laana ya aliyekuwa memba hai wa kundi hilo, marehemu Steven Kanumba kutokana na kumnyanyapaa enzi za uhai wake, Ijumaa linakupa mchapo kamili.
Marehemu Kanumba.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Kanumba alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa kundi hilo lakini kabla hajafa, yaliibuka majungu ambayo yalimsababisha ajiengue na kususia kundi hilo huku akiwa na kinyongo moyoni.

Wakilia juu ya kaburi la marehemu Kanumba.
“Kanumba hakufurahishwa na majungu yaliyokuwa yakiendelea ndani ya klabu dhidi yake, akajiapiza kwamba hatakaa akashiriki masuala ya kundi hilo hadi pale wahusika watakapojisafisha.
“Wakati sisi tukipanga yetu, Mungu naye anapanga yake. Kanumba alifariki wakati ambao wasanii waliomsukia majungu hayo hawajajisafisha, kama si kumuomba msamaha,” kilisema chanzo.
Staa wa filamu Bongo, Jackline Wolper.
KATIBU ASAKWA
Baada ya kunyaka maelezo hayo ya chanzo chetu, mapaparazi wetu walianza kuwatafuta waliokuwa viongozi wa klabu hiyo na kufanikiwa kumpata aliyekuwa katibu msaidizi, Devotha Mbaga, ambaye alikiri kwamba klabu hiyo ina laana ya Kanumba.
HUYU HAPA DEVOTHA
Akizungumza kwa hisia kali maeneo ya nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar, Devotha alisema mgogoro unaoendelea ndani ya kundi hilo ambalo linapumulia mashine baada mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na katibu wake, William Mtitu kujiuzulu ni laana ya Kanumba hivyo wanatakiwa kuomba radhi kaburini kwake.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Wema Sepetu.
Alisema enzi za uhai wa Kanumba baadhi ya wasanii ambao wanagombana chini kwa chini kwa sasa ndani ya kundi hilo (majina yapo), walimnyanyapaa na walikuwa wakimchukia na kufikia hatua ya kuwakataza wanachama wote kutoshiriki kwenye filamu zake.
“Ukweli baadhi ya wasanii hasa hao viongozi wanatakiwa kutambua makosa waliyomfanyia Kanumba enzi za uhai wake na wamuomba msamaha kwani walimkosea sana na wakishaomba, naamini Bongo Movie itasimama lakini wasipofanya hivyo hiyo laana itaendelea kuwatesa na watapigana kila siku.
“Yaani kuna wakati hadi huwa nafikia hatua ya kusema bora Kanumba alikufa mapema yawezekana Mungu alikuwa na kusudi lake maana angeaibika na angeonekana ni mtu asiyefaa katika jamii kutokana na mikakati ambayo wasanii wenzake walikuwa wameipanga,” alisema Devotha.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Stive Mengere.
KUMBE WALIWAHI KUKAA KIKAO
Kama hiyo haitoshi, katika aya nyingine, Devotha alisema kuna wakati waliwahi kuweka kikao cha kusameheana kilichoandaliwa na Ridhiwan Kikwete ambaye sasa ni Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini mambo bado yakawa ‘shagala baghala’.
“Nakumbuka kwenye kikao kimoja ambacho aliitisha Ridhiwan Kikwete kwa ajili ya wasanii na kusema kama kuna mtu amemkosea mwenzake wasameheane baada ya kuongea na sisi na kuondoka, watu walianza kuongea maneno mabaya ya kashfa na hapo ndipo walipopanga mikakati ya kumchafua na kutofanya kazi na Kanumba lakini baada ya siku chache alifariki.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'.
“Hao wanaogombana sasa hivi ndiyo walikuwa vinara katika kumnyanyapaa Kanumba na ndiyo haohao siku ya mazishi yake ndiyo waliobeba jeneza, msalaba na kuvaa suti wakati walikuwa hawako naye vizuri, unajua roho huwa haifi kwa hiyo wanatakiwa kuomba msamaha ili wawe na amani,” alisema Devotha.
NI LAANA NZITO?
Kwenye mazungumzo hayo na waandishi wetu, Devotha aliendelea kutiririka kuwa kutokana Kanumba kufariki dunia akiwa na kitu moyoni kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna kitu alikizungumza muda mchache kabla hajafariki au kuwa na kinyongo na Bongo Movie hivyo wasanii hao wanatakiwa kwenda kuomba msamaha kaburini kwake ili kundi hilo lisimame tena.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Dk. Cheni.
WAOMBA RADHI KIMYAKIMYA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba kuna baadhi ya wasanii wamedaiwa kuanza kwenda kaburini hapo kimyakimya na kuomba radhi ili kundi lao lirudi kwenye mstari kama lilivyokuwa enzi za marehemu Kanumba.
“Tumeona hali ni mbaya bora twende vinginevyo mambo yataharibika zaidi ya hapa,” alisema msanii mwenye taito kubwa ndani ya Bongo Movie kwa sharti la kustiriwa jina.
WENGINE KUOMBA RADHI
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya wasanii kwa sharti la kutotaja majina yao ambao walikiri kwamba mambo hayaendi sawa kutokana na laana ya Kanumba hivyo wako mbioni kwenda kuomba msamaha katika kaburi lake wakiamini uliokufa ni mwili roho ingali hai.
KUMBUKUMBU
Marehemu Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza-Vatcan akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Alizikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate