BONDIA
Floyd Mayweather amesema kwamba umri umeenda sasa na anakaribia miaka
40, lakini bado ana uwezo mkubwa ambao atauonyesha Jumamosi mjini Las
Vegas katika pambano la marudiano dhidi ya Marcos Maidana.
Wawili
hao walizipiga awali Mei mwaka huu, wakati Mayweather aliposhinda kwa
utata na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza pambano baada ya kupanda
ulingoni mara 46.
Mayweather,
mwenye umri wa miaka 37, amebakiza mapambano kadhaa kabla ya kustaafu,
lakini amesema hakuna jinsi angekwepa kupambana na mkali wa Argentina,
Maidana kwa mara ya pili baada ya watu kuomba sana pambano la marudiano
baina yao.
"Ninafahamu
ninakaribia miaka 40, lakini bado nina nguvu," amesema Mayweather.
"Bado ninajisikia vizuri na ninataka kwenda huko kupambana. Ninakwenda
kuwapa nyinyi watu kile mnachotaka kuona.
"Pambano la kwanza lilikuwa tamu tamu sana. Natumai pambano la safari hii pia litakuwa lenye mvuto zaidi," amesema.
No comments:
Post a Comment