EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 12, 2014

NUSU FAINALI DANSI 100% KUFANYIKA DON BOSCO SIKU YA KESHO


Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Simu aina ya Samsung E1205 yenye tochi na redio yenye thamani ya shilingi 25,000 tu.Zitakazopatikana katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu. Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Simu aina ya Samsung E1205 yenye tochi na redio yenye thamani ya shilingi 25,000 tu.Zitakazopatikana katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga,Kikundi kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Modem yenye ubora wa 3G inayouzwa kwa shilingi 25,000 tu katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.

Na Mwandishi wetu.
Kinyang’anyiro cha mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa  na kituo cha televisheni cha East  Africa(EATV) chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo hapo jumamosi hatua ya nusu fainali  inafanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 10 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.
Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambao yamefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho mpaka sasa ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The W.T,Tatanisha Dancers,Quality Boys,Wakali sisi, Mazabe Powder,Dar Crew na The winners Crew.
Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shamte,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha nusufainali hiyo watapata makundi 5 yatakayoingia  moja kwa moja kwenye fainali hapo baadaye.
“Huu ni mwaka wa tatu EATV tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.Kwa kweli mwaka huu mashindano haya yamekuwa na umaarufu mkubwa na ushindani wa hali ya juu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.
Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa  moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.
Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom itaendendelea kudhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Pia alitoa wito kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ili kuwapa moyo vijana watakaotoa burudani kali pia na kuweza kununua bidhaa mbalimbali za Vodacom zitakazopatikana kwa bei nafuu kabisa kiwanjani hapo kama vile Modem na Simu aina ya Samsung E1205 zote zikiuzwa kwa shilingi 25,000 tu”Alisisitiza Nkurlu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate