Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu
Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti
muigizaji mwenzao, Kajala Masanja kutokana na filamu fupi
aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na waandishi wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa
Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto
wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.
“Kitu ambacho nimekipenda ni kwamba filamu ni fupi lakini ujumbe
umeeleweka pia amefikiri kitu cha tofauti kabisa kwani hata watoto wa
rika zote wanaweza kuangalia kwa ajili ya kujifunza,” alisema JB huku
Ray akiunga mkono hoja.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment