EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 12, 2014

SITTA ASHUKIWA KAMA MWEWE




Dar es Salaam. 
Mpango wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta wa kutaka ya wajumbe wake walioko nje ya nchi kupiga kura kupitisha Katiba inayopendekezwa, umepingwa na wasomi, ukielezwa ni kinyume na kanuni za Bunge na sheria za nchi.


Wasomi hao, wanaharakati na wanasiasa wamesema Tanzania haina utaratibu wa raia wake kupiga kura wakiwa nje ya nchi na kwamba hiyo ni mbinu ya kufanya udanganyifu.

Juzi, Sitta alisema wajumbe wa Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa sababu zozote, ikiwamo ya matibabu na Hijja, watapiga kura hukohuko mara upigaji kura utakapoanza Septemba 26, mwaka huu na kuwataka wajumbe hao kuacha mawasiliano yao watakapokuwa nje na kwamba uongozi wa Bunge umeanza kufanya mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania, ili wawepo watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria kusimamia kazi hiyo.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema suala la Watanzania kupiga kura wakiwa nje ya nchi halimo kwenye kanuni zinazoongoza Bunge hilo na ni vizuri utaratibu huo ukaachwa.

Alisema anachokiona sasa ni Bunge kuendelea kupoteza fedha za wananchi wakati hakuna maridhiano huku uamuzi ukiwa umefikiwa kwamba Katiba Mpya itapatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema: “Hata kanuni za mabunge ya Jumuiya za Madola ambazo sisi tunazifuata ikitokea mjumbe anaumwa anapelekwa kwenye ukumbi wa Bunge kupiga kura, kura haipigwi sehemu yoyote.


“Hata katika Bunge la Uingereza ikionekana mjumbe anatakiwa kupiga kura lakini anaumwa atapelekwa ukumbini kwa msaada wa uongozi wa Bunge, ili aweze kutimiza haki yake ya kidemokrasia lakini haki hiyo haiwezi kumfuata huko aliko.

“Sitta analichukulia suala la Katiba kama lake binafsi, utaratibu wa kupiga kura za kificho haukubaliki kwa sababu utasababisha uchakachuaji,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema Tanzania haina utaratibu wa raia wake kupiga kura wakiwa nje ya nchi.


Mwanasheria huyo alisema kinachofanywa na Sitta kinaonyesha namna Bunge la Katiba linavyolazimisha mchakato huo.

“Kituo pekee cha wajumbe wa Bunge Maalumu kupiga kura ni ndani ya Ukumbi wa Bunge na si vinginevyo. Kinachofanywa na Sitta ni kuwahadaa Watanzania, mtu anaumwa atapigaje kura wakati hata kwenye majadiliano hakuwapo? Unalipigia kura jambo ambalo umeshiriki kwenye majadiliano,” alisema.

Alisema Tanzania haina utaratibu wa raia wake kupiga kura wakiwa nje ya nchi na kwamba endapo Serikali inataka kuuruhusu basi ifanye hivyo.

Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Felix Kibodya alisema kama kuna idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge Maalumu ambao wamesafiri kwenda nje ya nchi katika kipindi hiki, basi Bunge liahirishwe kama ambavyo wadau wamekuwa wakishauri.
“Nani atatuhakikishia usalama wa kura hizo, kama ni upigaji wa kura za siri nani atatunza siri hizo, tunajiuliza maswali mengi je, kutakuwa na msimamizi wa upigaji huo wa kura,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda alisema ingawa kuna nchi zenye utaratibu wa raia wake kupiga kura wakiwa nje ya nchi, Tanzania haina utaratibu huo.

“Sitta anafanya mambo ya ajabu kuanzisha utaratibu huo, hii inaonyesha mambo yameshakuwa magumu na sasa wanaokoteza kura popote zilipo,” alisema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Iringa, Profesa Gaudence Mpangala alisema Sitta anataka kuokoteza kura na kwamba Katiba ni suala la maridhiano na si wingi wa kura... “Ndiyo maana nimekuwa nikipendekeza Bunge Maalumu lisitishwe kwa sababu linapoteza fedha za wananchi,” alisema.

Wakili Peter Shayo wa Arusha alisema utaratibu wa kuwaruhusu wajumbe walioko nje ya nchi kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ni kukiuka kanuni za Bunge hilo.
“Ukisoma vizuri kanuni za hilo Bunge, kura za siri zinataka kuwapo kwa mawakala, nje ya nchi watapatikanaje? Maana ama anapiga kura ya ndiyo au hapana lazima kuwe na wakala anayemwamini, huko nje wanawapataje?” alihoji.

Hata hivyo, Mjumbe wa Bunge hilo, Charles Mwijage alisema haoni tatizo kwa wajumbe watakaokuwa nje ya nchi kupiga wakiwa huko... “Naamini Mwenyekiti (Sitta) na timu yake ya wataalamu wamezipitia hizo kanuni na kujiridhisha lakini usisahau kanuni pia zinaweza kufanyiwa marekebisho kama ni lazima.”
CHANZO: MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate