Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wahandisi
mbalimbali hawapo pichani kuhusu umuhimu wa Taaluma ya Uhandisi na
Maendeleo nchini kabla ya kufunga mkutano huo wa mwaka uliondaliwa na
Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB).
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa
na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Profesa Ninatubu Lema
wakawanza kushoto pamoja na Mbunge wa Tunduru kaskazini, Mheshimiwa Ramo
Makani wakikagua baadhi ya kazi zinazofanywa na wahandisi nchini.

Wahandisi
zaidi ya 200 wakila kiapo cha Uhandisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
Kisutu Waliyarwande Lema, huku viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.

Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikagua moja ya
mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania.

Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi zawadi ya
kompyuta laptop kwa mmoja kati ya wanafunzi wakike waliofanya vizuri
katika masomo ya kihandisi nchini.

Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipewa maelezo
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) Dkt. Leonard
Madaraka Chamuriho wakwanza kushoto kuhusu kazi mbalimbali za Baraza
hilo.

Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi
mbalimbali katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika
masomo ya Uhandisi nchini. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini–Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment