Stori: Mayasa Mariwata STAA
asiyekauka kwenye vyombo vya habari Bongo, Wema Sepetu ‘Beautiful
Onyinye’ amesema kuwa, hawezi kujishughulisha kamwe na mgogoro ulilipo
kwenye Klabu ya Bongo Movie Unity unaomtaka mwenyekiti wao, Steve
Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzuru.
Wema alifunguka alipokuwa akijibu swali lililomtaka aeleze mtazamo
wake juu ya mgogoro huo ambapo alisema anatambua kwamba hali si shwari
klabuni hapo huku baadhi ya wasanii wakidai mwenyekiti wao anachakachua
fedha za chama lakini kwa upande wake hataki kujiingiza na ishu na hiyo.
“Mh! Sio rahisi kabisa mimi kuingilia sekeseke hilo kusema eti Steve
anafaa kuendelea na madaraka au kuachia ngazi, sitaki kuingilia hilo
kabisa maana huwa sifatiliagi sana mambo ya Bongo Movie zaidi ya vitu
muhimu tu,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment