Mahaba mahabani! Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu
Hans amefunguka kuwa staa mwenzake ambaye ni mwandani wake, Vincent
Kigosi ‘Ray’ amefika kwenye penzi lake ndiyo maana ametulia kwani
amepata ‘malovee’ aliyokuwa akiyatafuta siku zote.
Chuchu alitoa kauli hiyo kwenye sherehe fupi ya kuzaliwa kwake
iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar ambapo
alikwenda kujumuika na watoto wachanga hasa wale waliofiwa na wazazi wao
pamoja na waliozaliwa siku hazijatimia ‘premature’.
Staa huyo alisema hivi sasa Ray hafurukuti kwake kwani anampa mapenzi
motomoto. “Hapa Ray amefika aambiwi kitu,” alisema Chuchu.Alipoulizwa
sababu ya kusherehekea hospitalini hapo aliweka wazi kuwa ilitokana na
yeye kuzaliwa ‘premature’ na mwanaye kumzaa akiwa ni premature hivyo
aliona awakumbuke watoto wa aina hiyo na waliozaliwa na kufiwa na wazazi
wao huku wakiwa wodini.
Chuchu aliyeongozana na wasanii kadhaa, aliwapatia watoto hao zawadi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment