Muonekano wa basi hilo.
ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Mohammed Trans leo lenye namba za usajili T 774 AWJ kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba wamelalamikia basi hilo kuwa ni bovu.
Sehemu ya mlango wa abiria.
Mmoja wa abiria ambaye hakutaja jina lake alionyeshwa kukerwa na basi hilo akilalamika kuwa mpaka leo asubuhi majira ya saa 1 asubuhi walikuwa bado Kahama wakisubiri basi hilo lilekebishwe tairi.
Basi hilo kwa mbele.
Mbali na kuwa basi hilo kuonekana kuchoka, pia abiria wamelilalamikia kuwepo kwa kunguni ndani ya basi hilo ambao huwasumbua hasa nyakati za usiku.
Tofauti na abiria hao abiria wengine waliosafiri na basi hilo Alhamisi ya Oktoba 16 kutoka Dar kwenda Bukoba nao walilalamikia huduma za kampuni hiyo wakidai kucheleweshwa katika stendi yao iliyopo eneo la Shekilango jijini Dar.
Abiria hao walidai kuchelewa kuondoka eneo hilo kama ilivyo kawaida muda wa saa 12:00 badala yake waliondoka saa 1:30 asubuhi baada ya kuambiwa kuwa basi lao ambalo ilibidi wasafiri nao lilikuwa na tatizo hivyo kuletewa hilo lenye namba tajwa hapo juu.
Abiria hao pia wakilalamika kuumwa na wadudu hao (kunguni) wakati wa safari yao hiyo.
Wasafiri hao wamezitaka mamlaka husika kuchukua hatua kabla basi hilo halijaleta maafa.
No comments:
Post a Comment