
Matumaini
ya watu wengi kumuona mshiriki kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba
la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa
baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa nje ya
jumba hilo.
Aliekuwa mshiriki wa Tanzania Laveda.
Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka
Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania
Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya
Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.

Laveda
anakuwa mshiriki wa sita wa jinsia ya kike kutolewa nje ya jumba la BBA
huku Alusa akiwa ni mshiriki wa kwanza wa kiume kutolewa Big Brother
Hotshots.
No comments:
Post a Comment