-Viongozi
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka
walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es
Salaam jana. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),
Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba
na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk. Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
Makatibu
wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada
ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa
Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na
Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
Mwanasheria
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa
Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.
Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa
kwenye mkutano huo.
Waendesha bodaboda ambao ni wafuasi wa Ukawa wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya Jangwani.
Vijana
wa chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba
yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com
No comments:
Post a Comment