EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, November 7, 2014

ANASWA! NJEMBA ADAIWA KURUBUNI WAKE ZA WATU KINGONO

Dustan Shekidele, Morogoro
Mji wa Morogoro umekumbwa na matukio mfululizo ya mafumanizi ambapo baada ya ticha wa shule ya msingi kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa kubondwa kwa kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa upadri kufumaniwa, mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la njemba mwenye asili ya Kiarabu limetokea.

Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed.
Kwenye Kata ya Mazimbu mjini hapa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Hemed, anadaiwa kunaswa laivu na mke wa mtu kwenye chumba anachoishi kilichopo Mtaa wa Boma mjini hapa.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi.
Wakinamama hao wakifanya juhudi kumtoa mke wa mtu (mwenye sidiria) eneo la tukio.
Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’ (umati), Hemed alidaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwarubuni na kumwaga fedha mbuzi kwa wake za watu na kuserebuka nao ndani ya ‘geto’ lake jambo lililowafanya wenye wake zao kumwekea mtego ambao ulipofyatuka ukamnasa majira ya saa 3:00 asubuhi.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa kwa jina moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Mashuhuda wa tukio hilo wakipiga chabo dirishani kwa mwarabu aliyenaswa.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwenye eneo la tukio, mume wa Husna aliyejitambulisha kwa jina moja la Siri alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimuaga mke wangu nakwenda Mwanza kwenye shughuli zangu za biashara. Nikiwa Mwanza nilijulishwa na majirani kwamba mke wangu kila siku anaacha watoto wetu kwa mama yake na kwenda kulala kwa Mwarabu.
Raia wenye Hasira kali wakiwa eneo la tukio.
“Ukweli kama mwanaume nilipatwa na hasira, nikatafuta ndege nikarudi hapa (Morogoro).
“Nimeelekezwa kwa Mwarabu na jamaa waliokuwa wamemwekea mtego, nilipofika nilichungulia dirishani, nikamuona mke wangu na Mwarabu wakiwa kitandani.
“Nilihisi kupooza mwili na roho ilikuwa inaniuma sana.”
Mwarabu(mwenye koti jekundu) aliyenaswa na mke wa mtu akiwa chini ya ulinzi.
Aliongeza: “Mimi na mke wangu tumefunga ndoa ya Kiislamu, tuna  watoto wawili, mmoja ana umri wa miaka mitano na wa pili ana mwaka mmoja na miezi saba.
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
Mtuhumiwa (mwarabu) akichukuliwa kwa mahojiano zaidi.
Kwa upande wake Husna ambaye alisitiriwa na wanawake wenzake waliokuwa wakimficha, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alimjia juu mwanahabari wetu na kumtolea maneno ya shombo.
Naye Mwarabu huyo alipohojiwa, pia alimtolea vitisho ‘kamanda’ wetu.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.

Baadaye viongozi wa Kata ya Mazimbu wakiongozwa na Afisa Mtendaji, Brioht Sospeter na polisi mmoja walifika eneo la tukio wakawaondoa wawili hao na kuwapeleka ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate