EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, November 23, 2014

HAPATOSHI: WABUNGE WA UPINZANI WADAI RIPOTI IMECHAKACHULIWA

Hali ni tete. Ndiyo neno ambalo unaweza kulizungumza kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mji wa Dodoma tangu juzi umejaa pilikapilika zikiambatana na mikutano iliyokuwa ikijadili kashfa hiyo.


Kamati ya Uongozi wa Bunge, Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa CCM, Baraza la Mawaziri, kwa nyakati tofauti walikaa kujadili ripoti ya escrow ambayo inatarajiwa kujadiliwa na Bunge Jumatano na Alhamisi.


Leo kikao cha wabunge wa CCM kinatarajiwa kufanyika kujadili suala hilo. Wabunge walionekana kila kona ya Viwanja vya Bunge jana wakijadiliana katika vikundi kuhusu sakata la escrow, huku wengine wakitaka hata miswada yote iliyobaki isijadiliwe ili kutoa nafasi kuichambua kwa kina kashfa hiyo.


Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo.




Wabunge wa CCM wamegawanyika katika makundi matatu; linaloshinikiza waliohusika na wizi huo wajiuzulu, kundi la watu wasiokuwa na msimamo na kundi linalotaka ripoti isijadiliwe bungeni.


Kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja iliyokuwa imepangwa awali.

Kamati ya Uongozi CCM

Katika kikao cha Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa CCM, wabunge wawili akiwemo Naibu Spika, Job Ndugai walipewa kibano kuhusiana na matamshi yao kuhusu sakata hilo.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa waliokumbana na kibano hicho ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, ambao waliambiwa kwamba matamshi yao wakati wakichangia yalilenga kukifanya chama hicho kuonekana kuwa ni cha wezi.

“Ndugai yeye walimbana kwa nini aliruhusu mjadala huo bungeni,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Aidha, baadhi ya wabunge wana hofu kuwa mjadala huo huenda usiende bungeni.

“Kuna taarifa kuwa Serikali bado haitaki mjadala huu uingie bungeni na wanamtumia Spika Anne Makinda kuukwamisha. Sisi hatuwezi kukubali uzuiwe kujadiliwa tutapiga kura za kutokuwa na imani naye iwapo atajaribu kufanya hivyo,” alisema mmoja wa wabunge kutoka Kanda ya Kati.

Alisema taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mahakama inataka kuzuia mjadala huo usiingie bungeni.

Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alitoa msimamo mkali kuhusu sakata hilo la escrow na kwamba ametaka hatua zichukuliwe kwa wahusika wote.
Katika kikao hicho inaelezwa kwamba Nchemba alionyesha msimamo wake waziwazi kuwa sakata hilo ni hujuma  na kwamba haiwezekani walioiba fedha hizo wakaachiwa tu hivihivi.

Ndani ya kikao hicho imeelezwa kuwa Mwigulu alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.
Alisema haiwezekani watu wakawajibika tu kwa kujiuzulu kwa kuwa huko ni kutoa tu likizo mtu akale mabilioni yake, hivyo wachukuliwe hatua ipasavyo na kufilisiwa.
“CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe,” alisema Mwigulu.

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe, zifilisiwe na fedha zirudishwe kwa wananchi.

Pia aliagiza mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha irudi serikalini.

Habari za uhakika kutoka kikao hicho zinaeleza kuwa Mwigulu aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri Mkuu na kusema kuwa kujiuzulu siyo adhabu stahiki kwa wizi mkubwa kama huo.

Mwigulu alisema: “Tazama wanafunzi, watoto wa maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna, maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia maskini?”
Kwa mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 bilioni Mwigulu akatoa agizo:

“Nimemwagiza Kamishna wa Kodi amfukuze kazi yule mtumishi wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe na wahusika wakamatwe.
“Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga maskini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini,” Mwigulu alisisitiza.

Wapinzani wadai ripoti imechakachuliwa
Kambi Rasmi ya Upinzan Bungeni, imedai kuwa watu wanaotuhumiwa kuhusika na uchotaji wa fedha katika akaunti ya  Tegeta Escrow, wamenyofoa baadhi ya nyaraka katika ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Ofisi ya Katibu wa Bunge.

Wakizungumza mjini Dodoma jana, viongozi hao walisema watuhumiwa wamekuwa wakisambaza nyaraka hizo  feki maeneo mbalimbali ili kuzima mjadala wa wizi huo usiingie bungeni.
“ Wanatoa nakala na kuzisambaza mtaani wakiwaaminisha watu kuwa ripoti haina kitu, hivyo hakuna haja ya kupeleka bungeni kujadiliwa,”alisema Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika.

Alisema kutokana na kubaini  njama hizo, kambi ya upinzani imetoa taarifa kwa Katibu wa Bunge na tayari mtu mmoja amekamatwa akihusishwa na upatikanaji na usambazi wa ripoti hiyo.

“Sisi tumeshuhudia akikamatwa mtu huyo aliyekuwa na nyaraka hizo, tunaliomba Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina na kumhoji uhusiano wake na watu wanaotuhumiwa katika ripoti hiyo,”alisema Mnyika
Kwa upande wake, Waziri Kivuli wa Fedha,  James Mbatia alitaja kurasa zilizonyofolewa katika ripoti hiyo kuwa ni zilizobeba mambo ya msingi ambazo ni ukurasa wa 57, 58 na 59.
“Tutaitisha kikao cha dharura kabla ya Jumatatu ili kushinikiza mjadala huu ufanyike kabla ya mambo mengine kwanza,”alisema Mbatia.
Mbatia alimuonya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutojaribu kuuzuia mjadala, ili kuepusha machafuko kama yaliyotokea katika nchi nyingine duniani.
Naye Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rajab Mbarouk Mohamed, aliwataka wananchi watakaoziona ama kupewa nakala za ripoti hiyo kufikisha katika vyombo vya sheria.
 “Wananchi wasiwe na wasiwasi sisi tuko imara katika kuhakikisha haki inatendeka, watuhumiwa wanakamatwa, wanafikishwa mahakamani na kurejesha fedha walizochukua,”alisema.
CREDIT: MWANANCHI JUMAPILI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate