EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, November 17, 2014

RIPOTI CAG BALAA

RIPOTI ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 200, kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umeanika madudu mazito yaliyofanywa na vigogo wa Serikali, Tanzania Daima limedokezwa.
Ingawa ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima limebahatika kuiona, imekwepa kutaja majina ya vigogo hao na taasisi wanazotoka, lakini inaonyesha kuwa jumla ya fedha za Escrow ni sh bilioni 306 ambazo ni matokeo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kulipishwa tozo la uwekezaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa.

CAG katika ripoti hiyo, anasema Tanesco walipaswa kurejeshewa sh bilioni 321 zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002 – 2012.
“Hivyo fedha za Escrow ni fedha za umma, yote ilipaswa kurudi Tanesco na shirika kuendelea kuwadai IPTL sh bilioni 15,” alisema CAG.
Madudu mengine yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ni kwamba, kampuni ya PAP haikununua kihalali hisa 70% za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwani zilizuiwa na Mahakama, hivyo hawana hati halisi za hisa na PAP ilifanya udanganyifu katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uwongo na kuikosesha Serikali Mapato ya sh bilioni 8.7.
Inaeleza kuwa, kosa hili linahusu pia mamlaka ya TRA Ilala, ambao walihusika kufanya mauzo hayo.
Akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM), ilifunguliwa na mmoja wa wabia wa IPTL, James Rugemalira, ambaye alikuwa akimiliki asilimia 30 ya IPTL huku kampuni ya Mechmar Bhd ya Malaysia ikiwa na hisa asilimia 70.
Kutokana na kiasi hicho cha hisa, Rugemalira amelipwa kiasi cha dola milioni 75 (Shilingi Bilioni 123), zikionyesha kwamba alilipwa kiasi cha dola milioni 7.5 (Shilingi bilioni 12.4) mwaka jana na kiasi kilichosalia alimaliziwa mwaka huu.
Kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa Rugemalira na kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh, ambaye kwa sasa ndiye mmiliki pekee wa IPTL baada ya kununua hisa za Mechmar na zile za VIP.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo Gazeti hili imeinasa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Gavana wa Banki Kuu (BoT), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, walivunja sheria kwa kuelekeza kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye tozo la uwekezaji isilipwe na kusababisha serikali kupoteza mapato ya sh bilioni 21.
“Waziri kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, hawakufanya utafiti wa kini kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya IPTL. Katibu Mkuu alisaini kutoa fedha za Escrow bila kuhakikisha fedha za Tanesco zinarudi, hivyo kusababisha upotevu wa zaidi ya sh bilioni 321,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Kwa upande wa Tanesco, Mkurugenzi wa Shirika hilo na Bodi yake, hawakutimiza wajibu wao kwa kugeuza maamuzi yao (ama kwa kushinikizwa na Wizara au kwa rushwa), na kulikosesha shirika hilo zaidi ya sh bilioni 321.
Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaririwa bungeni kwamba fedha hizo sio za umma, ripoti hiyo inaonyesha kuwa ni za umma.
Mgogoro uliosababisha fedha kuwekwa katika akaunti hiyo ya Tegeta ya BoT, ulitokana na Tanesco kugoma kulipa gharama za uwekaji mitambo (Capacity Charge), kwa IPTL mwaka 2006 kwa vile ilibainika IPTL ilikuwa ikitoza gharama kubwa kuliko iliyopaswa.
Akaunti hiyo ya Tegeta, ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande hizo mbili umalizike.
Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina ya wamiliki wa IPTL na Tanesco umemalizika na hivyo Benki Kuu haina sababu ya kuhifadhi fedha hizo tena.
Uamuzi huo wa kulipwa, ulizua upinzani mkali bungeni ambapo wabunge wawili wa kambi ya upinzani; Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, walidai kuwa zoezi hilo limejaa ufisadi na Bunge liliazimia kwamba suala hili lifanyiwe uchunguzi wa kina na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate