EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, November 18, 2014

SANGOMA AZIMIA AKITOA MAJINI!

CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
INASHANGAZA sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida mganga wa kienyeji ‘sangoma’ mmoja aliyefahamika kwa jina la Lambalamba amejikuta akiingia kwenye hatua ya nusu kifo kufuatia kupoteza fahamu baada ya kuelemewa na majini aliyokuwa akiyatoa shuleni.
Sangoma mwenye usongo mwekundu akiingia kazini na timu yake kutuliza majini.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Kiluvya - Madukani jijini Dar es Salaam kwenye Shule ya Msingi Makurunge ambapo sangoma huyo aliitwa kuyatoa majini yaliyokuwa yakiwafanyia mauzauza wanafunzi na walimu.
ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakisikia sauti za ajabuajabu shuleni hapo hali iliyokuwa ikiwafanya wasome kwa hofu. “Hali hiyo ilipozidi baadhi ya wanafunzi wakaenda kuwaambia wazazi wao ambao nao walipopeleleza kwa baadhi ya walimu walihakikishiwa kwamba ni kweli shuleni hapo kuna majini yanawasumbua wanafunzi na walimu pia,” alisema shuhuda huyo.
Timu hiyo ya ‘Sangoma’ ikimwamtoa mbuzi kafara kwa ajili ya zoezi hilo.
Ili kuwanusuru wanafunzi kutoka kwenye mauzauza hayo, wazazi waliweka kikao cha dharura na kuamua kuandika barua kwenye ofisi za serikali ya mtaa ili kuomba kibali cha kuitwa sangoma mkali, mwenye sifa, anayejua majini, afike shuleni hapo kuyafukuza.

Ilidaiwa kuwa mauzauza ya shuleni hapo ni wanafunzi wakienda chooni husikia vilio vya watoto wachanga au paka lakini hawaonekani. Wakati mwimgine hupatwa na hali isiyoweza kuelezewa kwa lugha sahihi.
‘Sangoma’ hao wakimsaidia mmoja wao aliyezidiwa na nguvu za majini.
SANGOMA ATINGA
Ikazidi kudaiwa kuwa, serikali ya mtaa japokuwa haiamini ushirikina, iliwaruhusu wazazi hao kutekeleza azma yao lakini serikali isihusike kwa lolote litakalotokea. Siku ilifika, sangoma huyo akaitwa, akiwa na wasaidizi wake wawili, alitia timu kwenye eneo hilo na kujigamba kuwa, tabu ya majini imekwisha!  Yeye ndiye Lambalamba bwana!
ATAKIWA MBUZI MNONO
Habari zinasema kuwa, ili kazi ifanyike kwa ufanisi na kuweza kuleta tija na ili wanafunzi hao wampe tano kwa kazi, sangoma huyo alitaka mbuzi mnono kwa ajili ya kumchinja ili damu yake imwagikie eneo hilo na majini kukimbia.
‘Sangoma’ wakiendelea kutoa msaada kwa mwenzao aliyeshambuliwa na majini.
Mbuzi alifikishwa, maandalizi ya uchinjaji yakafuatia huku sangoma akianza kusema maneno ya ‘kitaalam’ kuashiria kuwa sasa kazi imeanza, majini yakae tayari kwa kukimbia eneo la shule.
HALI TETE
Ikazidi kudaiwa kuwa, wakati sangoma akisemasema maneno yake ya kufukiza, ghafla alianza kuyumbayumba mpaka kujikuta yupo chini kisha  akatulia tuli licha ya wananchi, wakiwemo wanafunzi kumpigia makofi.
‘Sangoma’ akiwa hoi maada ya kushambuliwa.
WASAIDIZI WAHAHA
Ilibainika baadaye kwamba, sangoma huyo aliyekuwa amelala chali kama kwenye msalaba alikuwa amepoteza fahamu hivyo wasaidizi wake walianza kuhaha kwa kummwagia maji ndoo nzima ili azinduke kama siyo kurejea kwenye uhai wake (pichani).

CHA AJABU SASA
Cha ajabu sasa, sangoma akiwa hajitambui chini na wasaidizi wake wakiendelea kumzindua, msichana mmoja ambaye hakujulikana jina mara moja, alianza kupagawa, akaishiwa nguvu huku akisemasema maneno yasiyoeleweka, watu ‘waliokula chumvi nyingi’ wakasema amekumbwa na majini.
Mmoja ya raia waliokuwa wakishabikia akiwa hoi baada ya kupigwa na majini.
“Huyo naye ni majini yamemvaa. Huenda yalipokuwa yanatolewa na mganga mengine yakahamia kwake,” alisema mzee mmoja bila kutaja jina lake. Ilibidi wasaidizi wa sangoma huyo wahamie kwake ili kumnusuru na janga hilo ambapo baada ya muda, msichana huyo alirejea katika hali yake ya kawaida.
HALI YATULIA, ZOEZI LASITISHWA
Baada ya sangoma naye kuzinduka, zoezi la kuyatoa majini shuleni hapo lilisimama huku mikakati ikiwekwa kwamba shughuli hiyo itaendelea tena siku kadhaa mbele.
Baadhi ya raia wakishudia yaliyojiri eneo la tukio.
MWENYEKITI WA MTAA ANENA
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiluvya-Madukani, Adelaida Bruno alisema yeye alipelekewa barua ya maombi kutoka kwa wananchi wake wakimtaka awaruhusu kumuita sangoma kwa ajili ya kuwasaidia kuondoa mambo hayo ya mauzauza shuleni hapo. “Mimi kama serikali, hatuamini ushirikina, niliipokea hiyo barua, nikawaambia kama wamekubaliana kumwita sangoma kuwasaidia basi wafanye wao wenyewe. Na siku hiyo ya sangoma sikuhudhuria,” alisema mwenyekiti huyo.

MWALIMU MKUU ATUPIA KAMATI
Uwazi lilimtafuta mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina ambapo alisema siku ya tukio hakuwepo lakini alisikia kutoka kwa watu na kama ni ukweli utakuwepo kwenye kamati ya shule.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate