Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk.
Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.
NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za
makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika
kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa
ukaribu katika maboresho na kukuza juhudi za mashirika binafsi ya sekta
ya afya.
Hayo yamesemwa leo Novemba 24 mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk.
Margaret
Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando
wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa
mwaka wa TPHA, katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.
Dk.
Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau
sekta binafsi wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea
kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya
msingi hususani masuala ya afya.
"Tunaipongeza
TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya
afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano
kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika
mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.
Aidha, aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe alisema
kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na huku
likitarajiwa kumalizika Novemba 28 mwaka huu ambapo wataalamu wa afya
na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
Naye
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano
hilo ni la kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa afya na mambo ya jamii
kutoka serikalini na mshirika binafsi ambapo watajadili changamoto za
ukuaji wa sekta hiyo ya afya na maboresho yake kwa pamoja sambamba na
kupata ujuzi watakaofanyia kazi.
"Kongamano hili la kisayansi la 31, ambalo kwa
mwaka
huutukiwa tunakutana ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa
mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii" alisema Dk.Kisanga.
No comments:
Post a Comment