THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu
za Tiba za Rais zakamilika.
Taratibu za
matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu hizo
za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya
leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini
Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Hata hivyo,
Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum
inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya
kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu
kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea
nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete
aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa
afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia
upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete
anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona
haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
24 Novemba,2014
No comments:
Post a Comment