Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara. Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye . Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo aliwaambia CCM inaimarika kutokana na kuwa na sera zenye kuleta maendeleo kwa Watanzania pamoja na kuthamini amani iliyopo nchini.(Picha na Adam Mzee)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mibure ambacho kinajengwa na mafundi wa kawaida wa kijijini hapo. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa kata ya Chienjele wilayani Ruangwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Chienjele wilaya ya Ruangwa ambapo aliwaambia vijana kuwa bado kuna fursa nzuri nchini katika kuleta maendeleo. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCMkata ya Nandagala wilayani Ruangwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji kwenye mto Ole kijiji cha Ng'au kata ya Mnachu wilaya ya Ruangwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Ng'au Ole wilaya ya Ruangwa ambapo aliwahimiza kutunza mazingira kwa kutokata miti badala yake wapande miti kutunza vyanzo vya maji. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nandagala ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoa wa Lindi.
No comments:
Post a Comment