EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, January 16, 2015

DIAMOND AMDUNGA MIMBA ZARI!


Stori: waandishi wetu/Ijumaa
BAADA ya kufunguka kuwa zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ wamegoma kumzalia, habari ya mjini kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni kwamba anadaiwa kumdunga mimba mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’, Ijumaa linakupa ubuyu wa motomoto.
Mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’.
CHANZO CHAVUJISHA MCHAPO
Wiki mbili zilizopita, chanzo kilicho karibu na Diamond kiliwalipenyezea mchapo mapaparazi wetu kuwa uhusiano wa Zari mwenye maskani yake Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ na jamaa huyo tayari umejibu hivyo mashabiki wa mastaa hao wategemee ujio wa uzao wa wawili hao.
“Hivi habari ya Zari kuwa mjamzito mnayo? Mbona iko wazi na Diamond amefurahi sana maana si unajua tena alihangaika sana kupata mtoto kwa Wema, Jokate na Penny wote wakamzingua? Sasa habari ya mjini ndiyo hiyo,” kilidai chanzo hicho huku kikiomba chondechonde kistiriwe jina.

DIAMOND ATHIBITISHA KIAINA
Wakati wanahabari wetu wakiendelea kuchimba undani wa habari hiyo, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, Diamond alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram iliyoashiria kwamba anathibitisha yale yaliyovujishwa na chanzo chetu kuwa yana ukweli.
PICHA ILIKUWAJE?
Picha hiyo aliyoitupia Diamond ilikuwa ikimuonesha mtoto wa kike, Zari akiwa amelala kwenye mapaja ya Diamond ikiwa imeambatanishwa na picha ya ‘Ultrasound’ kuonesha tumbo la Zari lina kiumbe kilichoanza kurutubishwa.
Picha ya ‘Ultrasound’ ikionesha tumbo la Zari kuwa na kiumbe ndani yake.
ASINDISIKIZA NA UJUMBE
Chini ya picha hiyo, Diamond alisindikiza na na ujumbe ulisomeka hivi:
“I can not wait to have you on my hand...# Chibu_Junior.”
(Siwezi kusubiri kukubeba mikononi mwangu Chibu Mdogo)
AITOA MTANDAONI
Katika hali ya kushangaza, wakati wapenda ubuyu wachache wakiwa ‘wameshaiiba’ picha hiyo mtandaoni, Diamond aliitoa fasta ikidaiwa kuwa alishauriwa kufanya hivyo.
“Atakuwa kashauriwa aitoe maana si unajua tena Wabongo wangeanza kumshambulia, akaona bora atoe fasta,” aliandika mmoja wa wadau wa Diamond mtandaoni.
ZARI NAYE ATUPIA
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Uganda, mara baada ya Diamond kuposti picha hiyo, Zari naye aliichukua na ‘kui-repost’ katika akaunti yake kisha na yeye kuitoa baada ya muda mfupi.
YAWA GUMZO UGANDA
Baada tu ya Zari kuposti na kuitoa picha hiyo, vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vikijadili picha hiyo na kufanya mastaa hao wawe gumzo nchini humo huku wadau mbalimbali wakitoa maoni yao.
“Tunampongeza Diamond kwa kuunganisha undugu kati ya Tanzania na Uganda, kama wamekubaliana wazae tu hakuna shida,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki mtandaoni juu ya ishu hiyo.
Shemeji yetu kwa 'Diamond Platnumz', Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ akijiachia.
DIAMOND ANASEMAJE?
Wanahabari wetu walimuibukia kwa zaidi ya mara tano Diamond nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar lakini hakuwepo, baadaye alipatikana kwenye simu na kujibu kwa kifupi:
“We kama umeona kwenye akaunti yangu unauliza nini tena?”
MTU WA KARIBU
Ili kuzidi kuchimba ukweli wa habari hiyo, wanahabari wetu walimvutia waya mtu wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda kuanika jina gazetini lakini akakiri kuwa Zari ana mimba ya Diamond.
“Mbona kitambo tu, Diamond alivumilia kwa muda mrefu lakini jana usiku (Jumanne kuamkia Jumatano) ndiyo akaamua kuweka picha kisha akaitoa,” alidai mtu huyo wa karibu na Diamond.
KUMBUKUMBU
Kabla ya habari hiyo ya mimba ya Zari, huko nyuma Diamond aliwahi kuambiwa hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke lakini mwenyewe alifafanua kwamba wachumba wake wote ‘aliobanjuka’ nao kwa nyakati tofauti, waligoma kumzalia kwa kile alichokiita ni kupenda ‘utoto wa mjini.’
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate