Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
 Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu akielekea katika
 kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama 
hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
 Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105 
waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani 
Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani
 tuheshimiane. 
 Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa 
chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana 
walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza
 kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa 
fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo 
ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu 
wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na 
shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na 
utulivu.
Akizungumza Ndugu Kinana alisema kuwa chama cha CUF
 hakitendi haki katika suala zima la demokrasia, ''kwani kila mtu ana 
uhuru wa kuhamia chama anachotaka na haitaji kubugudhiwa,hivyo Viongozi 
wa CUF,wanapaswa kulitambua hilo na kuwaacha wananchi waamue watakavyo 
ili mradi hawavunji sheria za nchi wala kumbugudhi mtu'' alisema Kinana.
Kinana
 yupo katika ziara ya siku tano ya Kikazi kisiwani Pemba,akihimiza na 
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni 
pamoja na kukagua uhai wa chama kisiwani humo.
 Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa  Maskani ya tawi la 
CCM-Tuheshimiane katika kijiji cha Mnarani Makangale,Micheweni mkoa wa 
Kaskazini Pemba.

 Baadhi
 akina mama Wakulima wa Mpunga wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa 
CCM,Ndugu Kinana aliyekwenda Bonde la Mpunga Koowe kuangalia na 
kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.
 Pichani
 kati ni Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji maji-Pemba Mbarouk Ali Mgau 
akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda bonde la 
Mpunga Koowe-wingwi, kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia 
maji chumvi katika bonde hilo.Afisa Mbarouk alieleza kuwa mradi huo 
umegharibu kiasi cha shilingi Milioni 170 zilizotolewa na TASAF.
 Ndugu
 Kinana akiwa na baadhi akina Mama ambao ni wakulima wa zao la Mpunga 
katika Bonde la Koowe,wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi 
katika bonde hilo
 Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimia na Mganga Mkuu wa Wilaya ya  
Micheweni,Dkt.Rashid Daud mara baada ya kuwasili katika hospitali ya 
Wilaya ya  Micheweni,Kaskaini pemba mapema leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizingumza na baadhi ya Madaktari wa hospitali ya Wilaya ya 
Micheweni,mara baada ya kuwasili katika hospitali hiyo,Kaskazini Pemba mapema leo. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya 
Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba, wanaoshuhudia ni madaktari viongozi 
mbalimbali wa wilaya ya Micheweni na hospitali hiyo. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 akipata maelezo kutoka kwa  Dkt.Rashid Daud Mkasha Mganga Mkuu wa Wilaya
 ya Micheweni wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa wodi katika 
hospitali hiyo. 
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika 
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Majenzi mjini Micheweni. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kweny uwanja wa Majenzi mjini Micheweni. 
 Katibu
 Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi 
wa chama cha CCM,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Shaame 
Mata,Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba mapema  leo.Pichani 
kulia ni Mbunge wa Viti maalum Pemba,Mh Maida Hamad Abdalllah na kushoto
 ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba
 
 
 
 
 
 
 














 
No comments:
Post a Comment