Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akizozana na polisi muda mfupi 
kabla ya kukamatwa pamoja na wafuasi wengine 32 wa chama hicho jijini 
Dar es Salaam jana. 
 Mwenyekiti
 wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akiwa chini ya ulinzi,eneo la Mtoni 
Mtongani jijini Dar jana,baada ya  Polisi kusitisha maandamano ya chama 
chake.
 ====== ======  ========
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam 
limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti 
Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano 
ambayo si halali.
                
              
Awali polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa 
yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu 
kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara 
yalifanywa na vyombo vya usalama.
                
              
Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya 
Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati
 ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja 
wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.
                
              
“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba 
tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano 
ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo 
na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya 
kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
                
              
Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano 
hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili 
yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna 
uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si 
halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.
                
              
Alisem sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo 
ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi
 hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko 
mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.
 
 
 
 
 
 
 


 
No comments:
Post a Comment