EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, January 20, 2015

MFANYABIASHARA AUAWA KWA RISASI GETINI

STORI: WAANDISHI WETU/Uwazi MFANYABIASHARA mwanamama aliyetambulika kwa jina la Prisca Paul Rugeiyamu au Mama Koku (34) ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi nje ya geti la nyumba yake huku mwanaye Careen (12) akishuhudia.
Padri akiuombea mwili wa marehemu Prisca Paul Rugeiyamu kanisani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Januari 12, mwaka huu saa mbili usiku maeneo ya Tabata Segerea jijini Dar ambapo kwa mujibu wa chanzo, Prisca alikuwa akirejea nyumbani kwake ndani ya gari aina ya Vitz baada ya kukusanya mapato yake ya siku kutoka kwenye biashara zake.

Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini.
Akiwa nje ya geti  la nyumba yake akisubiri kufunguliwa, ndipo majambazi walitokea ghafla wakiwa kwenye pikipiki na kulizunguka gari hilo na kutoa bastola wakitaka wapatiwe fedha na laini za mitandao ya simu alizokuwa akizitumia katika biashara yake ya huduma za kifedha kwa njia ya simu katika moja ya maduka yake.
Waombolezaji wakiwa ni wenye huzuni kaburini.
Chanzo hicho kilisema kuwa, Prisca alibishana na majambazi hao kwa muda ambapo walimpiga risasi ya mguuni na kumuongeza nyingine baada ya kuendelea kugoma kutoa fedha.
“ Walimpiga risasi nyingine sehemu za tumbo na kuchukua fedha zinazodaiwa kufikia shilingi milioni arobaini na tano huku mwanaye Careen akishuhudia tukio hilo baada ya kufungua geti hilo kwa ajili ya kumpokea mama yake,” kilisema chanzo.
Waombolezaji wakiweka taji la maua kwenye kaburi la marehemu.
Inaelezwa kuwa Careen baada ya kuona hayo alikimbilia kwa bibi yake ambaye ni mama mzazi wa Prisca anayeishi jirani na nyumba yao aliyefika eneo la tukio ambapo majambazi hao waliokuwa wakijiandaa kutoweka walimpiga risasi ya mguu mama huyo na kuondoka kwa kasi.
Hata hivyo, baada ya majirani kufika eneo hilo walimchukua Prisca na kumkimbiza Hospitali ya Amana lakini alifariki akiwa njiani na maiti  yake ikahifadhiwa hospitalini hapo.
Mtoto wa marehemu akishika picha ya mama yake.
Akizungumza na waandishi wetu, ndugu wa familia hiyo anayejulikana kwa jina la Geofrey Frank alisema kuwa baada ya kifo chake walishangaa kuona wafanyabiashara wa madini wakija katika msiba na kudai kuwa Prisca alikuwa mfanyabiashara mwenzao, na kuongeza kuwa marehemu hakuweka wazi kazi yake hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo marehemu alikuwa mfanyabiashara wa madini, mmiliki wa duka la vocha za jumla, duka la vifaa vya ujenzi na mmiliki wa duka la vinywaji maeneo ya Segerea.
Marehemu Prisca Paul Rugeiyamu enzi za uhau wake.
Amewaacha yatima watoto watatu, mkubwa  ana miaka 12  huku wengine ni mapacha wana miaka saba. Mwili wa marehemu ulizikwa Januari 15, mwaka huu katika Makaburi ya Segerea jijini Dar.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate