EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, January 9, 2015

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAENDELEA KUPUNGUA

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Desemba, 2014 leo jijini Dar es salaam.Wengine ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja (kushoto) na Johnson Nyella, Meneja Utafiti wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
8/1/2015.Dar es salaam.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.8 iliyokuwepo mwezi Novemba kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Taifa leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula zikiwemo Mahindi, Unga wa mahindi, mbogamboga, mihogo ,sukari ,Mafuta ya taa, dizeli, petroli na Simu za kiganjani kumechangia kupunguza mfumuko wa bei nchini
Amesema kuwa wastani wa Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwaka mzima kutoka Januari hadi Desemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 6.1 kutoka asilimia 7.9 uliokuwepo kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2013.
Ameeleza kuwa Tanzania  inaendelea kufanya Vizuri katika nchi za Afrika Mashariki katika kudhibiti Mfumuko wa bei kwa kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti viashiria vinawezakuchangia kuwepo kwa mfumuko wa bei.
 
Akitoa ufafanuzi kuhusu mfumuko wa bei katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Kwesigabo amesema kuwa umekuwa na mwelekeo unaofanana, Kenya ukipungua na kufikia asilimia 6.02 mwezi Desemba kutoka 6.09 za mwezi Novemba na Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.1 za mwezi Novemba, 2014.
Aidha, amesema mwenendo wa Fahirisi za bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini katika kipindi cha  mwezi Desemba 2014 amesema kuwa Fahirisi hizo zimeonyesha kuongezeka hadi kufikia150.92 kutoka 150.54 za mwezi Novemba 2014.
Amefafanua kuwa kuongezeka kwa Fahirisi hizo kunatokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo mchele, unga wa mahindi, samaki, matunda jamii ya machungwa, mbogamboga, mavazi ya wanaume na wanawake na viatu vya wanaume.
Kwa upande wake Meneja Utafiti wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Johnson Nyella ameeleza kuwa kuendelea kupungua kwa Mfumuko wa Bei nchini kunatokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kupitia Benki hiyo kwa kuangalia utekelezaji wa Sera na Mipango ya maendeleo.
 
Amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na utulivu wa Uchumi kwa kipindi kirefu, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikifuatilia mwenendo wa bei katika Soko la Dunia, bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini na ufuatiliaji wa mwenendo wa uchumi wa nchi zinazoizunguka Tanzania.
Amesema malengo ya muda mrefu ya  Benki kuu ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa Mfumuko wa bei unapungua na kufikia asulimia 5.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate