Polisi nchini Los Angeles inasema 
kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight 
amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na
 gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.
 Polisi
 wanasema kuwa Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha
 magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Polisi
 wanasema kuwa Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha
 magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur
 
 
 
 
 
 
 

 
No comments:
Post a Comment