 
X wa Zari, King lawrence akipozi.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo 
alisema mara nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli
 katika mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi 
huyo wa zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake,
 kitu ambacho  ni cha kijinga.
Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini 
kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua 
kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi,  anatafuta 
nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond 
na kuongeza:
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Zari.
“Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza katika mitandao zaidi 
ya mimi na Zari, ningemshauri aendelee na shughuli zake za kila siku, 
asihangaike na kitu asichokijua, kugombana na mimi ni sawa na kumpigia 
mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili niweze kuitangaza nchi yangu, 
yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha jina lake, siwezi kubishana 
na mpuuzi.”Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa akiweka picha zake, Zari na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya mkali huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana kuwa ni kushikwa na wivu.
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment