EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, January 19, 2015

NI LAZIMA MUACHANE KWA UGOMVI?

Nianze kwa kumshukuru Maulana kwa kunijalia kuiona siku hii ya leo nikiwa mzima wa afya. Ni matumaini yangu kwamba na wewe msomaji wangu uko poa kabisa, karibu jamvini tubadilishane mawazo na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi.
Imewahi kukutokea kwamba licha ya kuwahi kumpenda au kupendana na mtu fulani, imefika hatua mambo yote hayawezi kuendelea tena, moyo umekinai, hisia zimekufa na jambo pekee unalotaka litokee ni wewe na mwenzi wako kuachana?

Kwamba huamini kama kuna jambo lolote linaloweza kuwafanya mkaendelea kukaa pamoja tena, dunia yenu ya mapenzi imefika mwisho na hakuna tena cha ziada! Hakuna kipindi kigumu kama hiki, hasa kama mtu unayeachana naye uliwahi kumpenda au yeye aliwahi kukupenda.
Kuangukia katika penzi la mtu fulani siyo jambo gumu ingawa hakuna jambo gumu kama kuachana na mtu. Wengi huwa wanashindwa kuukubali ukweli, matokeo yake wanasababisha matatizo ambayo yangeweza kuzuilika mapema.
Sishauri watu waachane isipokuwa nachotaka kujadiliana na wewe msomaji wangu ni namna bora inayoweza kutumika kumaliza penzi ambalo haliwezi tena kuendelea. Tunashuhudia kila siku watu wakiachana kwa matatizo makubwa, wakifanyiana ugomvi mkubwa, kupigana, kutukanana, kutoleana kashfa za kila aina, eti kisa mapenzi yamefika mwisho.
Unafikiri ni sawa kuachana kwa vurugu kiasi hicho wakati mliwahi kuishi pamoja kwa amani, upendo na mahaba ya nguvu? Nini huwa kinasababisha baadhi ya watu wanakuwa na tabia za aina hii?
HUO SIYO MWISHO WA MAISHA
Inapotokea umefanya kila kitu kulitetea penzi lako lakini imeshindikana, ni busara kuukubali ukweli kwa sababu mwisho wa mapenzi siyo mwisho wa maisha. Huwezi kujua Mungu anakuepusha na nini, kubaliana na hali halisi kwa sababu inatokea na wewe siyo wa kwanza kuachwa au kukataliwa na umpendaye.
Cha msingi ni kujitahidi kutulia, maumivu yapo tena makali lakini ni vyema kujua namna ya kukabiliana na hali hii ngumu bila kusababisha matatizo zaidi. Mlikutana kwa amani, mkapendana lakini penzi lenu halikupangwa kudumu, kubali matokeo na usonge mbele bila kumfanyia mwenzi wako vurugu.
MPE HAKI YAKE
Kingine ambacho kinatajwa kusababisha ugomvi kwa wanandoa au wapenzi walioishi kwa kipindi kirefu wanapoachana, ni mgawanyo wa mali au vitega uchumi vilivyopatikana mkiwa pamoja.
Wanaume ndiyo wanaotajwa zaidi kuwanyanyasa wanawake wanaoachana nao kwa kukataa kabisa kugawana vitu vilivyochumwa pamoja. Hakuna haja ya kukomoana, mpe haki yake ili na yeye huko anakokwenda, akayaanze vizuri maisha yake.
Kubalianeni wenyewe nani achukue kitu gani, hakuna haja ya kupelekana mahakamani au kuanza kusumbuana kwa vitu ambavyo mnaweza kuvimaliza kwa kutumia busara. Narudia tena kusema kuachana ni jambo baya linaloumiza lakini kuna muda huwa unafika, mnakosa njia nyingine mbadala zaidi ya kuachana.
Kama mlijaliwa kupata watoto, kubalianeni jinsi ya kuendelea kuwalea watoto bila matatizo. Kubaliana na ukweli na maisha yataendelea, jipe moyo kwamba huenda utampata mwingine ambaye ni bora kuliko huyo unayeachana naye.
Kwa leo niishie hapo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri. Kama una ushauri au kuna lolote ambalo ungependa kulijua, tuwasiliane kwa namba za hapo juu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate