STAA wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ amemshauri msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupigania kuolewa na mwandani wake, Nuhu Mziwanda ambaye alimvisha pete ya uchumba siku chache zilizopita kwa kuwa kitendo hicho kwa sasa kimeshazoeleka.
Staa wa muziki wa mduara Zuwena Mohammed ‘Shilole’akivikwa pete na mwandani wake, Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Sandra alisema anafagilia sana mapenzi ya wawili hao kwani anaona wanaendana pamoja na utofauti wa umri uliopo anamtaka Shilole ahakikishe anaolewa haraka iwezekanavyo kwani hata mwanadada Wema Sepetu alivishwa pete ya uchumba na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mpaka sasa hawajafunga ndoa malengo yao yameishia njiani.
No comments:
Post a Comment