EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, January 18, 2015

WAZIRI MAGUFULI ATANGAZA KUKAMILIKA KWA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA (KM 60)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe akiteremka kukagua tuta la barabara ya Ndundu –Somanga (KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami. Sehemu ya barabara ya Ndundu –Somanga (KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami. Mhandisi wa Mkoa wa Lindi Eng. Isack Mwanawima akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe.

Wanahabari wakimhoji Dereva wa basi la abiria kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kuhusiana na kukamilika kwa sehemu ya barabara hiyo.
WAZIRI wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kukamilika kwa barabara ya Ndundu- Somanga (Km 60) na kuwataka wakazi wa mikoa ya kusini kuitumia vizuri barabara hiyo kuibua fursa za kiuchumi na hivyo kujiletea maendeleo.
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa barabara hiyo uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe.
“Wito wangu kwenu wakazi wa mikoa ya kusini ni kuitunza barabara hii ili idumu kwa muda mrefu na kuibua fursa za kiuchumi zitakazo wawezesha kupata maendeleo na kupunguza umaskini” alisisitiza Waziri Magufuli.
Kufatia kukamilika kwa barabara hiyo, Dkt. Magufuli ameishukuru Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Barabara Nchini, (TANROADS), kwa kazi kubwa ya kusimamia kazi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali.
“Nampongeza Katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kwa usimamizi makini uliosababisha kukamilika kwa mradi huu muhimu utakaoleta ukombozi kwa wakazi wa mikoa ya kusini” alisema Waziri Dkt.Magufuli
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe ameelezea kuridhishwa kwake na ujenzi wa barabara hiyo na kuwaomba wananchi kuitunza ili idumu kwa muda mrefu.
“Barabara hii imekamilika kwa kuchelewa lakini imezingatia viwango vilivyowekwa kimkataba hivyo nawasihi madereva na wananchi kuitumia kwa uangalifu ili kuepuka ajali na kuibua fursa za maendeleo” alifafanua Eng. Iyombe
Barabara ya Ndundu-Somanga ni sehemu ya barabara kuu ya Dar-Es-salaam -Lindi-Mtwara ambayo imekuwa kwenye matengenezo kwa muda mrefu na Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 60.
(Habari na picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate