EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, February 14, 2015

LEO NDIYO LEO VALENTINE’S DAY, DAR LIVE!

Makala: Andrew Carlos
HATIMAYE ila siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapendanao wote ‘Valentine’s Day’ imefika ambapo leo, Februari 14, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar kutafuka moshi wa burudani kutoka kwa wakali wa mapenzi, Christian Bella ‘Obama’ pamoja na Mfalme Mzee Yusuf.
 
Mkali wa masauti, Christian Bella ‘Obama’.
Good newz kwa wapendanao ni kwamba mkali wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ atazindua ngoma yake mpya ya mapenzi kwa mara ya kwanza inayojulikana kama Nashindwa ikiwa ni zawadi maalum kwa wapendanao wote watakaofika huku Mzee Yusuf akiendeleza malavidavi.
Katika makala haya, yanabainisha utamu zaidi utakaopatikana usiku wa leo.
WAKALI WA BENDI
Haina kupepesa kuwa upande wa muziki wa Dansi, bendi inayobamba kwa sasa kwa kufanya shoo kibao za kufa mtu ni Malaika Music iliyo chini ya Christian Bella.Kuonyesha ni usiku spesho kwa wapendanao, Malaika Music watahakikisha wanawapagawisha wapendanao wote kwa kuimba na kucheza nyimbo zao zote kali za mapenzi kwa staili ya Kizaire na Kibongo.
Nalo kundi linalotikisa kunako miondoko ya Taarab, Jahazi Modern litatanda jukwaa zima la Dar Live likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf.Jahazi watakuwa na wakali kama Leila, Mishi, Fatuma Mcharuko, Mwansiti, Amigo na wengine kibao wakiwapa raha za Kipwani wapendanao.


RED CARPET
Mbali na kuwepo kwa zawadi maalum kwa kapo itakayotoka bomba zaidi. Wapendanao wote watapata fursa ya kupiga picha ‘red carpet’ na wakali watakaotumbuiza, Bella pamoja na Mzee Yusuf.

WAKALI WA MAPENZI
Je unajua wakali wa nyimbo za mapenzi wanapokutana pamoja nini kinatokea? Basi leo Dar Live, Mfalme Mzee Yusuf na Jahazi wataanza kwa kulitetemesha jukwaa kwa nyimbo zao kali zote za mapenzi.
Miongoni mwa nyimbo zitakazofunika ni Tiba ya Mapenzi, Wapendanao, My Valentine, Mpenzi Chocolate pamoja na wimbo mpya ambao ni habari nyingine kwa sasa wa Mahaba Niue.
Bella naye atapanda na Malaika kuonyesha kuwa ni hatari kwa nyimbo za mapenzi kwa kuuzindua wimbo wake mpya wa Nashindwa sambamba na kupiga ngoma zake zote kali kama vile Safari Siyo Kifo, Msaliti, Nakuhitaji, Yako Wapi Mapenzi pamoja na wimbo uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
SAPRAIZ KIBAO
Umeshawahi kubadilishana namba za simu na mastaa? Basi kwa mara ya kwanza Bella atabadilishana namba za simu na wapendanao wote sambamba na kuzungumza nao mawili matatu.Nafasi nyingine ambayo ni nadra kuipata kwa staa yoyote itatokea leo, ambapo mastaa kibao wakiongozwa na Bella watajumuika na wapendanao kupata vyakula mbalimbali, nyama choma, vinywaji na vingine vingi vitakavyokuwepo ukumbini hapo.
 
Mfalme Mzee Yusuf.
BELLA KUFUNIKA JUKWAA
Bella amewahakikishia wapendanao wote watakaofika watashangaa historia atakayoiandika usiku wa leo.“Siyo kama najisifia! Hapana, ila ukizungumzia kati ya wasanii wote Bongo iwe ni wa Taarab, Dansi, Bongo Fleva, Vigodoro ama muziki wowote, hakuna msanii ambaye anafunika jukwaani kama mimi.
Nikipanda tu jukwaani nasomba mashabiki wote, hata kama walikuwa wamelala, wapo mbali wote wanahamia kwangu na kuimba nao pamoja. Wapendanao wajiandae kwa kufanya maajabu ya aina yake jukwaani.”
***
MSANII AJIVUNIA KUFANYA KAZI NA NATURE
Stori: Mikito Nusunusu
BWA’MDOGO anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Hassan  Ridhiwan ‘Perfect Rymes’ amefunguka kuwa anajifunia kufanya kazi na legendari wa muziki huo, Juma Kassim ‘Nature’ kwani ni wachache sana wanaoweza kupata bahati hiyo.
Akizunguza na Mikito Nusunusu, Perfect Rymes alisema kitendo cha yeye kufanya wimbo wa Sindanganyiki katika Studio Uprise Music kwake  ni chachu ya kufanya vizuri hivyo atazidi kukaza ili atusue.
“Muziki unahitaji kupatambana ili uweze kufanikiwa, kuanza kufanya kazi na mkongwe kama Nature ni hatua nzuri kwangu, niwaombe mashabiki wanipe sapoti naamini nitatoboa,” alisema Perfect Rymes.
***
KEISHA: INAUMA WANATUUA KAMA KUKU!
Stori: Laurent Samatta
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hadija Shaban ‘Keisha’, amefunguka kuwa anaumia kuona watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanaendelea kuuawa kama kuku wakati kila siku elimu inatolewa.
Keisha ametumia sana kipaji chake kufikisha ujumbe kukemea mauaji hayo lakini anashindwa kuelewa ni kwa nini kesi za mauaji ya albino zimekuwa zikicheleweshwa.
“Tunaumia sana hiki ni kilio chetu cha muda mrefu sana lakini bado mambo yanaendelea, nakosa hata imani na mamlaka zinazohusika,” alisema Keisha.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate