EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, February 14, 2015

STARA THOMAS AFUMANIWA!


Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah/Risasi  GPL
HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzikazti alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’.
Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas akiwa na mumewe.
Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam.
FUMANIZI LILIVYOTOKEA
Akilisimulia Risasi Jumamosi baada ya kuulizwa kama kweli fumanizi lilikuwepo, mume wa Stara alifunguka hivi: “Ni kweli ilitokea. Siku ya fumanizi nilikuwa nimesafiri, lakini nikarudi ghafla bila kumpa taarifa mke wangu.
“Nilikuwa nyumbani, yeye hakuwepo. Saa 9:00 usiku ndiyo nilimwona Stara akirejea tena akiwa amelewa. Aliletwa na gari mpaka nje ya nyumba.”

NDANI YA GARI KWA NUSU SAA
“Lile gari lilisimama zaidi ya nusu nje bila kushuka mtu ndipo nikaamua kulifuata. Stara aliponiona akamwambia dereva ambaye najua ni jamaa yake, aondoe gari kwani mimi ni mume wake nitampiga.
“Nilizuia wasitoke, yule jamaa akarudi nyuma na kuniparuza kwenye mguu na tairi, nikadondoka. Niliposimama nikaokota jiwe na kulirushia gari nikavunja kioo cha mbele.”
STARA, JAMAA POLISI
Mume huyo anaendelea kusimulia: “Baada ya hapo Stara aliondoka na yule jamaa mpaka Kituo cha Polisi Tabata ambapo walinishtaki. Niliitwa polisi kwa madai ya uharibifu wa kioo.
“Kwa vile nilikuwa nasafiri kwenda nje ya nchi (ni dereva wa malori) niliona mambo yaishie pale kituoni, nilikwenda nikachukuliwa maelezo kisha nikalipa shilingi laki saba (700,000).”
Mume wa Stara Thomas Raumu Ally.
DALILI ZA KUVUNJIKA KWA HESHIMA
Habari zaidi zilidai kwamba, wawili hao wamekuwa kwenye ugomvi wa mara kwa mara.
Imeelezwa kwamba, ugomvi wao ulianza pale Raumu aliposhindwa kulipa ada ya shilingi laki tano ya mtoto wa Stara (jina tunalo) huku madai ya mchepuko nayo yakisambaa hali iliyokuwa ikishusha heshima ya familia.
TUJIUNGE NA RAUMU
Akifafanua kuwepo kwa sakata hilo pamoja na chanzo kizima, Raumu alisema kuwa Stara amekuwa akimfanyia vituko na mambo ya ajabu tangu aliposimamishwa kazi kwenye kampuni aliyokuwa akifanyia awali (jina kapuni) baada ya kutokea matatizo.
“Mimi ni dereva wa malori, nakwenda Lusaka (Zambia) na Congo (DR), nimekuwa na mgogoro na Stara baada ya kusimamishwa kazi. Unajua ukiwa huna kazi hata fedha huna. Alitaka nimlipie ada ya laki tano mtoto wake  lakini nikawa sina, ikawa maneno.”
KUMBE KUNA MENGINE ZAIDI
“Huwezi kuamini ndugu zangu wamenitenga mimi kwa sababu wakati naanza kuishi na Stara nilibadili dini yangu ya Kiislam na kumfuata yeye kwenye ulokole (wakati huo) halafu leo hii ananiletea mambo ya ajabu! Stara amuogope Mungu.”
WALIKUTANA HIVI
Akizungumzia historia fupi ya uhusiano wao, Raumu alisema walikutana kwa mara ya kwanza, Stara alikuwa  akisoma Shule ya Sekondari ya Mzizima, Dar, miaka ya 90.
Stara Thomas.
MAPENZI MOTOMOTO
Mapenzi yao yalikuwa motomoto lakini baadaye walipotezana kisha kuja kuonana tena miaka ya hivi karibuni huku kila mmoja akiwa na maisha yake.
Kutokana na namna walivyopendana kupita kiasi kipindi cha awali, wawili hao walirejesha uhusiano ambapo mwanaume huyo alihamia nyumbani kwa Stara, Tabata baada ya staa huyo kuachana na mumewe wa ndoa aliyezaa naye watoto wawili.
STARA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Stara ili kujibu tuhuma hizo ambapo alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Haloo Stara…
Stara: Haloo.
Mwandishi: Unamfahamu Raumu?
Stara: Kwanza wewe nani?
Mwandishi: Mimi ni mwandishi wa Global Publishers.
Stara: Ndiyo namjua Raumu.
Mwandishi: Ni nani kwako?
Stara: Ukitaka kujua kuhusu Raumu, njoo nyumbani tuongee.
Mwandishi: Nataka unijibu kuhusiana na tuhuma za yeye kukufumania.
Stara: Njoo nyumbani wewe na Raumu tuongee tuyamalize huku.
Hata hivyo, mwandishi wetu alitinga nyumbani kwa staa huyo lakini hakumpata hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate