Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Kariati Tractor ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Kwadelo, Omary Kariati (kulia), akisalimiana na Katibu wa Itikadi na
Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye alipofika
kuwakabidhi matrekta wakulima kutoka mikoa mbalimbali Dar es Salaam jana
mchana.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye akisalimiana na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili kwenye
hafla hiyo ya kukabidhi matrekta.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa (kulia), akimuelekeza jambo Nape.
Mjumbe
wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Dk.Edmund Mndolwa akijaribu kuendesha moja ya matrekta hayo.
Mwalimu Hamza Haji mmoja wa wanufaika wa mkopo wa matrekta hayo akizungumza na waandishi wa habari.
Mkulima Khalifa Kuluvi kutoka Kata ya Kwadelo akizungumza na waandishi wa habari.
Mhe. Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya Kampuni ya Kariati Tractor.
Baadhi
ya matrekta waliogaiwa wakulima hao pamoja Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa ambaye
amenunua ekari 100 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kilimo kwanza.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
(katikati), akijaribu moja kati ya matrekta saba aliyowakabidhi wakulima
wa mikoa kadhaa Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kutekeleza kilimo
kwanza. Matrekta hayo yanakopeshwa kwa wakulima mbalimba nchini na
Kampuni ya Kariati Tractor. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Kariati Tractor ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati
na kushoto ni Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund Mndolwa.
Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Kata ya
Kwadelo iliyopo Kondoa mkoani Dodoma wamemuomba Katibu wa Itikadi na
Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye awasaidie
kuwaombea serikali wamegewe kipande cha ardhi kwenye hifadhi ya Taifa ya
Mkongonelo ili wakitumie kwa kilimo.
Ombi hilo limetolewa kwa Nape na Diwani
wa Kata ya Kwadelo Alhaji Omary Kariati Dar es Salaam jana kwenye hafla
fupi ya kukabidhi matrekta saba ambapo Nape alikuwa mgeni rasmi.
" Mheshimiwa pamoja na jitihada hizo zote
za kamapuni yangu ya Kariati Tractor kuwawezesha wananchi wa kata yangu
kuwakopesha matrekta changamoto kubwa tuliyonayo ni ukosefu wa ardhi
iliyochukuliwa na serikali kwa ajili ya hifadhi ya Taifa ya Mkongonelo
tunakuomba utusaidie kutuombea Wizara ya Maliasili na Utalii watukatie
kipande cha kilomita mbili katika hifadhi hiyo kitumike kwa kilimo"
alisema Kariati.
Kariati alisema baada ya kupimwa kwa eneo
hilo maeneo yote yaliyokuwa yakitumika kwa kilimo yamechukuliwa na
serikali jambo lililosababisha wananchi kukosa mashamba.
Akijibu ombi hilo Nape alisema atalipeka
ombi hilo serikalini ili kuona namna watakavyosaidia na kuwa maeneo
mengi ya hifadhi za taifa yalipimwa kwenye miaka 1975 wakati idadi ya
watu ilikuwa ndogo ukilinganisha na sasa.
"Wakati yanapimwa maeneo haya idadi ya
watu ilikuwa kidogo lakini sasa idadi imekuwa ni kubwa hivyo ni vema
serikali ikaangalia mahitaji ya matumizi ya ardhi hiyo kwa wananchi na
kutenga mengine kwa ajili ya hifadhi" alisema Nape
Alisema mwenye uwezo wa kumaliza suala
hilo ni Serikali ya CCM ambayo imeshika dola na kuwa moja ya ilani ya
chama hicho ni kutekeleza kilimo kwanza kinachofanywa na diwani huyo na
washirika wake.
Nape alimpongeza diwani huyo na Mjumbe wa
Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Edmund
Mndolwa kwa kutekeleza ilani hiyo kwa vitendo kwa kununua ekari 100 kwa
ajili ya kilimo ambapo alisema angependa wajumbe wengine kuiga mfano huo
ambao ni ilani ya chama.
Diwani Kariati alisema kuwa matreka hayo
saba yaliyokabidhiwa kwa wakulima wa kutoka mikoa mbalimbali yanafikisha
idadi ya matrekta 100 yaliyokopeshwa kwa wakulima mbalimbali nchini na
kuwa mmoja wa watu walionufaika nayo ni walimu wanne akiwepo Mwalimu
Hamza Haji wa Shule ya Msingi ya Kwadelo.
Kariati alitoa mwito kwa walimu nchini
kujitokeza kwa wingi kukopa matrekta hayo ili kuinua uchumi wao na hivyo
kuondoa dhana potofu ya kuogopa kwenda kufanya kazi vijijjini kwa madai
ya kuwa na maisha magumu wakati wenzao wamepiga hatua ya maisha.
No comments:
Post a Comment