EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 11, 2015

DIAMOND APATA MSHTUKO DENI LA MIL.800

Musa Mateja/mchanganyiko MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuwepo madai ya kudaiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 na serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
ILIKUWAJE?
Mwishoni mwa wiki iliyopita, barua inayodaiwa kuandikwa na mamlaka hiyo halali ya serikali, ilisambazwa mitandaoni, ikielezwa kuwa ilikuwa imetumwa kwa meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ndiye yupo juu, ikimtaka kupeleka nakala za mikataba yote ya muziki aliyoingia kwa ajili ya kufanya shoo, kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.

GUMZO MITANDAONI
Baada ya kuwekwa kwa barua hiyo mitandaoni, watu mbalimbali walitoa maoni yao walionyesha hisia tofauti, baadhi wakipinga kwa madai kuwa wanamuonea huku wengine wakisema siyo Diamond tu, bali wasanii wote wanastahili kulipa kodi kutokana na mapato wanayopata kupitia kazi zao.

KODI ZIPOJE KIBONGOBONGO?
Mtaalam mmoja wa mambo ya kodi aliyezungumza na Risasi Mchanganyiko, alisema kwa mujibu wa taratibu zao, msanii huyo anastahili kulipa kodi kiasi cha asilimia kumi ya fedha anazopata katika kila mkataba anaoingia.

“Kuna walipa kodi wengine kama wafanyabiashara, hawa wanalipa kile ambacho kitaalamu kinajulikana kama Capital Gain, yaani kulipa kadiri unavyopata. Mtu anakwenda TRA mwenyewe na kueleza mapato yake na mamlaka itampangia kiasi cha kulipa. Ila watu kama wasanii na wengine wanaolipwa, wanatakiwa kutoa asilimia kumi ya malipo,” alisema mtaalam huyo aliyekataa kutajwa jina gazetini.
DIAMOND ANADAIWA SH. NGAPI?
Kama suala hilo litafanyika kwa mujibu wa mtaalam huyo, Diamond ambaye malipo yake kwa shoo moja yanatajwa kuwa ni shilingi milioni 20 kwa sasa, atatakiwa kulipa kiasi kinachozidi milioni 800 kutokana na hesabu zilizofanywa na watu wanaofuatilia muziki wake.


“Jamaa anafanya wastani wa shoo kama tatu kwa mwezi hapa nyumbani (Tanzania) na tatu zingine nje. Zile za nje analipwa siyo chini ya dola 25,000 kwa shoo moja. Nadhani unajua kwa sasa huyu dogo ndiye anakimbiza sana katika soko, yupo juu na kila promota anahitaji huduma yake,” alisema mdau huyo wa Bongo Fleva.
MCHANGANUO ULIVYO
Kama hesabu za mdau huyo zitakuwa sawa, inamaanisha kuwa Diamond anaingiza wastani wa shilingi milioni sitini kwa mwezi hapa nyumbani, na milioni 127  kwa mikataba ya nje ya nchi (Dola moja ya Marekani ni sawa na shilingi 1700), ikimaanisha kuwa kwa mwezi mmoja, kijana huyo aliyekulia Tandale, anaingiza kiasi cha shilingi milioni 187.5.

JUMLA  YA MAPATO MIAKA MINNE
Kwa mahesabu hayo, Diamond Platnumz anaingiza wastani wa shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka, fedha ambayo ukijumlisha kwa miaka minne, ameweka kibindoni shilingi za kitanzania bilioni 8.8, ambazo asilimia kumi yake ni shilingi milioni 880, ambazo ndizo zinazotakiwa kulipwa.

MENEJA AFUNGUKA
Mmoja wa mameneja wa Diamond, Babu Tale alipotafutwa na gazeti hili na kuulizwa kama ni kweli alipewa barua au kujua kuwa barua hiyo ipo, alikataa kulizungumzia suala hilo, akisema siyo jambo la kulielezea kwenye vyombo vya habari.“Hata mimi nimeiona hiyo barua (anautaja mtandao wa kijamii maarufu sana nchini), sina cha kuelezea kwenye media,” alisema meneja huyo huku akikataa katakata kusema kama ameipata au la.

DIAMOND MWENYEWE SASA
Baadaye Risasi Mchanganyiko liliwasiliana moja kwa moja na Diamond mwenyewe, ambaye alikuwa nchini Nigeria, alikoenda kwa ajili ya shoo iliyoandaliwa na Africa Magic Viewers Choice Awards jijini Lagos, alishtuka sana na kuomba asizungumzie suala hilo.“Daah! Milioni 800? Anyway naomba nisizungumzie suala hilo kwa sasa.”

TRA WAIKANA BARUA
Gazeti hili lilipomtafuta ofisa wa TRA, ambaye jina lake limeandikwa katika barua hiyo, aitwaye Tillya V.M. T, alikanusha kuandika barua hiyo na kusema ni mambo ya kugushi yanayofanywa mitandaoni.
“Hakuna kitu kama hicho, its something created,” alisema bosi huyo akimaanisha kuwa jambo hilo ni la kutengenezwa.

NYOTA YA WEMA YAHUSISHWA
Wakati hayo yakijiri, baadhi ya wadau wamesema suala hilo linahusishwa na mojawapo ya kauli iliyowahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu kuwa mwanaume yeyote anayekuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi, nyota yake hung’aa, lakini anapoachana naye, hufifia.

WENGINE WAMHUSISHA ZARI
Aidha, wadau wengine walisema ishu hiyo huenda imeibuka kama mkosi uliochangiwa na kujiingiza katika mapenzi na mwanadada raia wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye mashabiki wanadai ni mtu mwenye mikosi, kwani Diamond ni mwanaume wake wa nne rasmi, wa tatu wa kwanza kila mmoja akiwa amezaa naye.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate