EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 12, 2015

LINAH ALAMBA MKATABA KINYWAJI CHA ‘JEBEL’

Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Brewers Ltd, Steve Gannon (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Linah (katikati) baada ya kukubali kusaini mkataba wa kuwa Balozi wa Jebel.  Kulia ni meneja wa Linah, Tonny Akwesa, akishuhudia makabidhiano hayo.
Linah (kulia) akisaini mkataba  huo na Mkurugenzi wa Serengeti, Steve Gannon, ndani ya ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi kuu za kampuni hiyo Temeke, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Linah na Mkurugenzi wa Serengeti Gannon wakionyesha kinywaji cha Jebel.
Steve Gannon akiangalia T-shirt yenye nembo ya kinywaji hicho mara baada ya kusainiwa na Linah.

…Akionyesha T-shirt hiyo baada ya kusainiwa na Linah.
Linah akiongea jambo kwa waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba.
Mkurugenzi Masoko wa Serengeti, Cescar Mloka (wa pili kulia), akifurahia jambo akiwa ameshikilia kinywaji hicho na Linah.  Wengine ni Tonny Akwesa na Steve Gannon.
Linah akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti.
…Akitambulishwa kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Serengeti akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumtambulisha Linah.
Linah akiwa na wafanyakazi wa Serengeti.
MSANII kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania  (THT) Estelinah Sanga ‘Linah’, leo ameingia mkataba  na Kampuni ya Serengeti Breweries Ltd, kupitia kinywaji chake cha Jebel.
Akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba huo, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Steve Gannon, alisema  wameamua kumpatia ubalozi wa kinywaji hicho Linah kufuatia uwezo wake mkubwa katika kuwashawishi wateja wao, na pia hiyo ni njia mojawapo ya kusapoti kipaji chake na itakuwa pia njia ya kushirikiana na wasanii wa Tanzania kwa kila kitu.
“Kampuni yetu imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Linah ikiwa njia  ya kutambua sanaa ya muziki Tanzania.   Serengeti Brewers Ltd kupitia kinywaji chetu cha Jebel, tumefurahishwa na uwezo wa Linah hivyo tunaamini kupitia kwake tutaweza kupata manufaa makubwa ya kutangaza kinywaji chetu cha Jebel,” alisema na kuongeza:
“Tunatarajia kuanza naye kazi rasmi kwa kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambayo ataifanyia katika nchi ya Kenya na Afrika Kusini.  Video hiyo itakuwa chini yetu, ila mkataba huu utambulike kwamba tunaanza na mwaka mmoja ingawa utakuwa endelevu zaidi.”
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate