Baraza
 la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika 
mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano 
ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .
Mwisho
 mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha
 kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  
na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu 
aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music 
Star wa Afrika
Mkurugenzi
 Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao 
Shalua katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za 
BASATA alisema”  Ushindi huu ni  furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa
 la Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa 
nchini  kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika 
kuwawezesha   vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua
 fulsa hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga
 kwa kufanya vizuri na kushinda mashindano haya. 
Nawashukuru
 sana Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu 
mashindano haya yaanze ikiwa ni kusajili  kampuni yao na kupata hati ya 
kufanya shughuli za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa
 mashindano haya na kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya 
kusafiri na kuagwa rasmi wakati wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya 
Afrika.  Kwakweli huu ni mfano wa kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa 
ujumla, kufata taratibu na kupata vibali maalumu pindi wanapoenda nje ya
 nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha nchi yetu.
Natoa
 wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili 
wa mashindano haya ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze 
kupata nafasi ya kushiriki na kuinua vipaji vyao. Aliongea Shalua
Akiongea
 kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw Jackson Mmbando 
alisema  Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano 
hili  tangu tulipolizindua.  tunampongeza sana mayunga kwa ushindi huu. 
Nalimi Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda marekani na kupata 
mafunzo chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video
 yake ya kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 
500,000/= Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon 
basi mayunga ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto
 zake.
Airtel
 ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia
 ushindi wake hapa nchini  na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya
 kazi na msaani nguli Akon.
Akiongelea
 ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia
 kura toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya
 pekee na naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio 
makubwa na mwanzo wa mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa 
mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi.
Nawashukuru
 Airtel  kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano 
wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu 
kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya 
yatakapotangazwa na kuanza .
Mashindano
 ya Afrika yalimalizika  kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza , 
Nigeria nafasi ya pili  na Congo Brazavile nafasi ya tatu.
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment