EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 30, 2015

KAJALA APEWA SIKU 5 ZA KUISHI

MASIKINI! Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni amejikuta akiwa katika wakati mgumu na wa hatari kufuatia watu wasiojulikana kuvamia nyumbani kwake na kutoa onyo kwamba wanampa siku tano tu za kuishi, Amani lina mkasa kamili.Ishu hiyo ya kushtusha ilitokea usiku wa saa nane ya kuamkia juzi, Jumanne nyumbani kwa staa huyo, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.
WALIKUWA KWENYE TOYOTA RAV 4
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watu hao wapatao watatu walitinga nyumbani hapo usiku huo mnene huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Rav 4 milango mitano rangi ya bluu ya kuiva na kumkuta mlinzi getini ambaye yupo kwa ajili ya kulinda usalama wa msanii huyo mwenye maadui kila kukicha.“Walikuwa watano, walikuwa kwenye Rav 4 milango mitano, rangi ya blue ya kuiva. Wakamkuta mlinzi, walimuuliza kama Kajala yupo, mlinzi aliwadanganya kwamba hayupo.”


MLINZI ALIJUA NI BWANA WA KAJALA
“Lakini mlinzi alidanganya akijua mmoja wa watu hao pengine ni bwana wa Kajala kwa hiyo ili kuua soo akasema hayupo lakini ukweli Kajala alikuwepo ndani. Yeye aliwaambia Kajala alikwenda kumsalimia mama yake, hajarudi.

WAACHA UJUMBE MZITO
“Ndipo mmoja wao akamwambia mlinzi kwamba, wao walikuwa na shida na Kajala lakini kwa sababu hayupo, wanaacha ujumbe apewe haraka sana. “Walisema akirudi aambiwe kuna watu walifika, wamempa siku tano za kuishi na kwamba wao wametumwa na mtu wa karibu na Kajala, lakini hawakumtaja kwa jina.
 “Yaani mlinzi alitumia akili sana na kuwaambia Kajala hakuwepo ndani, alikwenda nyumbani kwao, ndiyo ilikuwa salama yake,” kilisema chanzo hicho.

AMANI LAMSAKA KAJALA
Baada ya kuinyaka  nyeti hiyo, Amani lilimsaka staa huyo na kumuuliza kama kuna ukweli wa madai hayo.
Awali, Kajala aligoma katakata kukubali akisema hajui lolote lakini alipobanwa zaidi na kuambiwa mlinzi wake ndiye aliyenyetisha habari hiyo, alikiri.

Kajala Masanja akiwa kwenye pozi.
MSIKIE MWENYEWE
“Any way, ni kweli ishu imetokea usiku, lakini siyo saa nane, ilikuwa kama saa sita hivi. Mimi nilikuwa nimelala, nikaona simu yangu ikiita. Nilipoangalia ni mlinzi, nikapokea. Akaniambia kuna watu wamekuja, wamemwambia wametumwa waniletee ujumbe kwamba nimepewa siku tano za kuishi na wametumwa na mtu wangu wa karibu.

“Mimi sikuogopa, nilitoka hadi kwa mlinzi, lakini nilikuta gari imeshaishia zake. Kifupi ni kwamba katika watu si waoga ni mimi, unajua kwa nini? Naishi kwa kumtegemea Mungu sana. “Kwa hiyo siogopi japokuwa habari hizo zimenichanganya kupita kiasi, najiuliza ni mtu wangu gani wa karibu. Basi si mtu wa karibu bali ni adui yangu. Hivi hapa najiandaa kwenda Kituo cha Polisi Kijitonyama (Dar) kutoa taarifa kwa ajili ya tahadhari,” alisema Kajala.
Akaongeza: “Unajua wiki yote iliyopita nilikuwa kwenye harakati za kumalizia filamu yangu ya Pishu. Kwa hiyo hata usiku wa jana nilichelewa kurudi, ile naingia tu nadhani ndani ya nusu saa ndiyo watu hao walikuja, kama ningechelewa zaidi huenda ningekutana nao getini.”
ANAMHISI NANI?
AMANI: “Kajala wewe unajijua, unadhani nani anaweza kukutumia ujumbe kama huu miongoni mwa watu wako wa karibu?”

KAJALA: “Mh! Siwezi kumtaja hata kama kichwani yupo au wapo! Nitabaki kuwa na hisia zangu tu kwa sababu sina ushahidi. Ila kama ningewaona kwa sura hao watu na kuwatambua huenda ningeunganisha.”
Amani: “Huna mtu ambaye hivi karibuni mmetupiana maneno mabaya kwenye simu au laivu?”
Kajala: “Sina. Mimi nipo na watu wangu ni amani tu na ndiyo maana nachangayikiwa.”
Mpaka tunakwenda mitamboni, Kajala alisema ndiyo amewasili kwenye kituo hicho polisi akisubiri kusikilizwa.

CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate