Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya
mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki lililoandaliwa na Lucas
Lutanilwa.Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya
mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki timu ya Mazombi FC lililoandaliwa
na Lucas Lutanilwa.Mwakilishi
wa Timu ya Vijana Jogging Club akipokea zawadi ya fedha baada ya
kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto.Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akizungumza kabla ya
kuanza kwa mtanange huo kati ya Timu ya Mazombi FC na Sobibo FC.Washindi wa nne wakipokea haki yao pia.Washindi wa nne wakipokea haki yao pia.Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akifuatilia mpambano kati
ya Timu za Mazombi FC na Sobibo FC. Mazombi walifanikiwa kutaa ubingwa
baada ya kuifunga Sobibo 1-0.Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa () akikagua timu ya Mazombi FC kabla ya
mpambano kuanza.Mgeni
rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akikagua timu ya Sobibo FC
kabla ya mpambano kuanza.Timu ya Sobibo FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.Timu ya Mazombi FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.Mashabiki mbalimbali wa Gongo la Mboto wakifuatilia mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto.Baadhi
ya wachezaji na mashabiki na Timu ya Vijana Jogging Club wakishangilia
baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto.
MEYA
wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa jana alitoa zawadi ya pikipiki baada
kuvutiwa na ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchezo wa fainali wa
mpira wa miguu kugombea pikipiki aina ya Boxer.
Meya
Slaa alilazimika kutoa pikipiki hiyo baada ya timu za Mazombi FC na
Sobibo FC zote za Gongo la Mboto kuonesha ushindani mkali katika mchezo
wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Kampala Gongo la Mboto jijini
Dar es Salaam.
Slaa
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ameahidi kuwakabidhi
pikipiki mpya timu ya Sobibo FC ambayo ilishika nafasi ya pili katika
mchezo huo wa fainali ambapo timu ya Mazombi FC iliibuka mshindi na
kukabidhiwa pikipiki mpya aina ya Boxer iliyotolewa na muandaaji wa
mashindano hayo Lucas Lutanilwa.
"...Kutokana
na ushindani mkubwa uliooneshwa na timu zote mbili natamka kwamba hata
washindi wa pili Sobibo FC nao ninawazawadia pikipiki kama waliopata
wenzao ili kuleta kiu ya kupenda michezo zaidi kwa vijana wetu," alisema
Slaa akizungumza alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa mabingwa Masombi FC.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa pande zote mbili timu ya
Mazombi imefanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa pikipiki mpya baada ya
kuifunga Sobibo FC goli 1-0 lilipatikana dakika 70 ya kipindi cha pili
cha mchezo huo.
Timu
zote mbili pia zilikabidhiwa seti mojamoja ya jezi kwa kuweza kufika
fainali, hata hivyo washindi wa nne na tatu wa Mashindano hayo
yaliyopewa jina la Luta Cup walipewa zawadi za fedha taslimu kama
pongezi. Timu ya Vijana Jogging Club walifanikiwa kutwaa ushindi wa tatu
na kujinyakulia fedha taslimu katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment