EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, June 8, 2015

MAKOSA 10 MKATABA WA SIMBA, SINGANO

Ramadhani Singano ‘Messi’ akisaini mkataba wake na Simba.
Na Mwandishi Wetu
SAKATA kubwa linaloutikisa mpira wa Tanzania sasa ni ule mkataba kati ya kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba.Messi anasema mkataba wake unaisha 2015, lakini Simba inasisitiza mkataba wao na Messi unaisha mwaka 2016, jambo ambalo linazua tafrani kubwa.

Mkataba wa Simba na Ramadhani Singano ‘Messi’ unaoishia 2016.
Championi Jumatatu lina kopi ya mikataba yote miwili, ule wa Simba unaomalizika Julai, 2016 na ule alionao Messi unaofikia tamati Julai, 2015. Mikataba yote inaanza Mei Mosi, 2013.
Katika mchanganuo wa mikataba hiyo, inaonyesha kuna makosa kadhaa na saba kubwa ndiyo yanayoweza kumfanya mtu yeyote aingiwe na hofu.Hata kabla ya TFF kukutana na pande hizo mbili kesho Jumanne, Championi Jumatatu linaainisha makosa katika mikataba hiyo miwili.
Mkataba wa Simba na Ramadhani Singano ‘Messi’ unaoishia 2015.
Moja:
Fonts; yaani muonekano au aina ya herufi zinavyokaa. Ukiangalia mikataba yote miwili zinapishana. Maana yake ule wa Messi na ule wa Simba ni mikataba miwili tofauti kabisa. Kama Messi ana kopi, hiyo ni ya mkataba upi? Nani kachakachua? TFF watatoa jibu kesho.
Mbili:
Saini za Messi, Joseph Itang’are (Makamu Mwenyekiti wa Simba), Evodius Mtawala (Katibu Mkuu Simba), zimesainiwa tofauti chini ya mkataba. Kwingine saini ya kulia ni Mtawala, kwingine saini ya upande huo ni Mzee Kinesi.
Tatu:
Namba tano na sita zimekuwa tatizo katika mikataba yote miwili. Katika ule wa Simba unaoisha 2016, kuna sehemu inaonekana ilikuwa tano, imelazimishwa kuwa sita. Ule wa Messi unaoisha 2015, kuna sehemu sita, inaonekana wazi imelazimishwa kuwa tano!
Nne:
Sahihi ya mwanasheria Mutakyamirwa Phillemon iliyo katika mikataba yote miwili inaonekana kuwa na tofauti kubwa. Je, ipi hasa ni sahihi?

Tano:
Sahihi za Mzee Kinesi katika mikataba yote miwili inaonyesha tofauti kubwa pia. Mwenyewe anaweza kusema yake ni ipi?
Sita:
Mihuri ya Klabu ya Simba iliyogongwa katika mkataba wa Messi na ule wa Simba, iko katika sehemu tofauti kabisa, ukilinganisha mikataba yote miwili.

Saba:
Muhuri wa mwanasheria Mutakyamirwa Phillemon pia umegongwa tofauti. Kwenye mkataba wa 2016 umelala, ule wa 2015 umenyooka. Sasa ‘photocopy’ ya Messi inafanana na upi, je, wake ndiyo sawa au orijino ndiyo umechakachuliwa?
Nane:
Sehemu ya mwisho ya mkataba, moja mwanasheria kasaini kushuhudia mkataba huo Mei Mosi, 2013 na upande mwingine Juni Mosi, 2013. Mwanasheria alisaini mkataba mara mbili, au tarehe zilichakachuliwa. Kwa nini sasa?
Tisa:
Ukurasa wa mwisho wa mkataba ambao unakuwa na saini za Messi, Mtawala na Mzee Kinesi ndiyo unaonekana kuwa na matatizo mengi zaidi kwa kutofautiana kabisa kwa ule unaoisha 2015 na ule wa 2016.
CHANZO: GPL
Kumi:
Saini za Mzee Kinesi kwenye 2016 na ukurasa wa mbele wa 2015 zinafanana kwa maana ya kuwa na apostrophe (kimkato cha juu) pale kwenye jina Itang’are. Kimkato hicho cha juu, kinakosekana kwenye saini ya ukurasa wa mwisho katika mkataba unaoisha 2015!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate